Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Virus vya Nipah,jinsi vinavyosambaa,dalili na Tiba

Virus vya Nipah,jinsi vinavyosambaa,dalili zake na Tiba

Nipah virus (NiV) ni virus jamii ya zoonotic virus, hupitishwa kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu) na pia vinaweza kuenezwa kupitia chakula kilichochafuliwa au moja kwa moja kati ya watu.

Kwa watu walioambukizwa, husababisha matatizo mbalimbali ikiwemo tatizo la kupumua,kuvimba kwa ubongo(encephalitis mbaya) n.k. Virusi pia vinaweza kusababisha ugonjwa mbaya kwa wanyama kama nguruwe, na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi kwa wafugaji.

Ingawa virusi vya Nipah vimesababisha milipuko michache tu inayojulikana huko Asia, virusi hivi vimeambukiza wanyama wengi na kusababisha magonjwa na vifo kwa watu.

Virusi vya Nipah vilitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1999 wakati wa mlipuko wa virusi hivi kwa jamii ya wafugaji wa nguruwe huko Malaysia. Hakuna milipuko mipya iliyoripotiwa nchini Malaysia tangu mwaka 1999.

Pia ilitambuliwa nchini Bangladesh mwaka 2001, na karibu milipuko ya kila mwaka imetokea nchini humo tangu wakati huo. Ugonjwa huo pia umetambuliwa mara kwa mara mashariki mwa India.

Mikoa mingine inaweza kuwa katika hatari ya kuambukizwa, kwani ushahidi wa virusi umepatikana katika hifadhi ya asili inayojulikana (aina ya popo ya Pteropus) na spishi zingine kadhaa za popo katika nchi kadhaa, zikiwemo Kambodia, Ghana, Indonesia, Madagaska, Ufilipino, na Thailand.

Uambukizaji wa Virus vya Nipah

Wakati wa mlipuko wa kwanza uliotambuliwa nchini Malaysia, ambao pia uliathiri Singapore, maambukizi mengi kwa binadamu yalitokana na kugusana moja kwa moja na nguruwe wagonjwa au tishu zao zilizoambukizwa.

Maambukizi yanafikiriwa kutokea kupitia uchafu kutoka kwa nguruwe(secretions), au kugusana moja kwa moja na tishu za mnyama mgonjwa.

Katika milipuko iliyofuata nchini Bangladesh na India, ulaji wa matunda au bidhaa za matunda (kama vile maji ya mitende mibichi) yaliyochafuliwa na mkojo au mate kutoka kwa popo walioambukizwa ndicho kilikuwa chanzo cha uwezekano mkubwa wa maambukizi.

Maambukizi ya virusi vya Nipah kutoka kwa binadamu hadi kwa binadamu pia yameripotiwa miongoni mwa familia na watoa huduma wa wagonjwa walioambukizwa.

Dalili za maambukizi ya Virusi vya Nipah

Watu ambao wameambukizwa virusi vya Nipah huanza na dalili za mwanzoni kama vile;

  • Kupata Homa
  • Kupata Maumivu makali ya kichwa
  • Kupata Maumivu ya misuli-myalgia (muscle pain),
  • Kutapika
  • Tatizo la sore throat.

Kisha zikifuatiwa na dalili zingine kama vile;

– Kupata kizunguzungu

– Kuzimia/kupoteza fahamu

– Na dalili zote ambazo huonekana kwa mtu mwenye tatizo la encephalitis.

– Baadhi ya watu pia hupata dalili kama za pneumonia, au hali mbaya zaidi kwenye mfumo wa upumuaji( severe respiratory problems, including acute respiratory distress).

Encephalitis na mshtuko wa moyo hutokea kwa wagonjwa wenye hali mbaya zaidi, na kuendelea hadi kufikia hatua ya kukosa fahamu ndani ya masaa 24 hadi 48.

Incubation period: muda kutoka mtu kupata maambukizi hadi mwanzo wa dalili) inaaminika kuwa kati ya siku 4 hadi 14. Walakini, kipindi cha incubation huweza kuwa cha muda mrefu kama siku 45.

Matibabu

Kwa sasa hakuna dawa au chanjo mahususi za maambukizi ya virusi vya Nipah ingawa WHO imetambua Nipah kama ugonjwa unaopewa kipaumbele kwenye Mpango wa Utafiti na Maendeleo wa WHO. 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.