Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo cha Mtu kukohoa baada ya kula chakula

Chanzo cha Mtu kukohoa baada ya kula chakula

Baadhi ya watu hupatwa na tatizo la kuanza kukohoa mara tu baada ya kula chakula, Je hali hii hutokana na nini?

Katika Makala hii nimekuchambulia baadhi ya Sababu za Tatizo hili la kukohoa baada ya kula chakula, Soma Zaidi hapa..!!!

Chanzo cha Mtu kukohoa baada ya kula chakula

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huweza kupelekea ukapata tatizo la kukohoa mara tu baada ya kumaliza kula, na Sababu hizo ni pamoja na;

1. Kuwa na Mzio au Allergies juu ya vyakula flani,

Unaweza kuwa na allergies na baadhi ya vyakula,hali ambayo ikakufanya kila baada ya kula tu vyakula hivo ukaanza kukohoa.

Mara nyingi tatizo la mzio kwenye vyakula(Food allergies) hutokea pale ambapo mfumo wako wa kinga ya mwili kujibu kupita kiasi/overreacts kutokana na proteins kwenye vyakula.

(It occur when the body’s immune system overreacts due to proteins in foods.)

Hivi ni baadhi ya vyakula ambavyo unaweza kuwa na Allergies navyo;

  • Maziwa pamoja na bidhaa zote zenye maziwa
  • Mayai
  • Samaki
  • Baadhi ya Nyama,mfano ya mbuzi,ng’ombe,kuku n.k
  • Karanga
  • Ngano
  • Soya/Soybeans n.k

2. Kuwa na Ugonjwa wa Asthma

Hii sio sababu,ingawa kwa mgonjwa wa asthma anaweza kupata hali ya kukohoa zaidi hasa pale baada ya kula vyakula ambavyo ana allergy navo.

3. Kuwa na Tatizo la acid reflux,

Tatizo ambalo huhusisha tindikali kupanda kutoka tumboni kwenda kwenye umio la chakula,

Mtu mwenye tatizo la Acid reflux/GERD huweza kupata hali kama hizi;

  • Kuhisi kama kuna kitu kimekwama Kooni
  • Kupata Kiungulia
  • Kikohozi
  • Ugumu wakati wa kumeza kitu
  • Maumivu kwenye kifua au tumbo
  • Kutapika
  • Harufu mbaya kinywani
  • Kupumua kwa shida
  • Kukosa Usingizi n.k

4. Kuwa na tatizo la Dysphagia

Tatizo la Dysphagia hutokea wakati unapata shida ya kumeza kitu(difficulty swallowing)

Vidokezo vya kukusaidia Kuzuia tatizo la kukohoa baada ya Kula

Vidokezo vya Kuzuia Kikohozi Baada ya Kula ni vipi?

Mara tu unapogundua kichochezi au chanzo, utaweza kuunda mpango ambao unafaa kwako kuzuia kukohoa baada ya kula. Vidokezo vingine vya kusaidia vinaweza kujumuisha:

– Kula chakula kidogo na kutafuna vizuri

– Tumia dawa kama una matatizo kama vile Acid reflux/GERD, mzio kwa baadhi ya vyakula(allergies) n.k.

– Epuka vyakula au vitu vyote ambavyo una allergies navyo au ambavyo huweza kupelekea kuwa na tatizo la Acid reflux

– Usilale chini mara tu baada ya kula.

Hivo ni baadhi ya vidokezo muhimu vya kukusaidia kuzuia tatizo la kukohoa baada ya kula.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.