Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

China imemfuta kazi rasmi Waziri wake wa ulinzi Li Shangfu

China imemfuta kazi rasmi Waziri wake wa ulinzi Li Shangfu, miezi miwili baada ya kutoweka na kutoonekana hadharani, hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu kuondolewa kwake na wala hakuna Mtu aliyetangazwa kuwa anachukua nafasi yake.

Kufukuzwa kwake, kunafuatia kufukuzwa kwa Wakuu kadhaa wa kijeshi akiwemo Qin Gang ambaye aliondolewa nafasi ya Waziri wa Mambo ya nje mwezi Julai mwaka huu.

Kufukuzwa kwake kunaiacha China bila Waziri wa Ulinzi huku ikijiandaa kuwakaribisha Maafisa wa ulinzi wa kigeni mjini Beijing wiki hii, Reuters iliripoti mwezi uliopita kwamba alikuwa chini ya uchunguzi juu ya tuhuma za rushwa akuhusishwa ununuzi wa vifaa na silaha kutokea Urusi.

Mara ya mwisho alionekana hadharani tarehe 29 Agosti, 2023 katika kongamano la usalama la Beijing na mataifa ya Afrika, Mhandisi huyo wa anga ambaye alianza kazi yake katika kituo cha kurushia satelaiti na roketi, Jenerali Li amekuwa na mwenendo mzuri wa kupitia safu ya Wanajeshi na Wasomo wa kisiasa wa China.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.