Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Katika kila vifo 3 nchini, kifo kimoja kinasababishwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza

#NasahaZaOdoUmmy #AfyaNiUtajiri – Yatupasa kila mmoja wetu katika kupigania maisha yetu ya kila siku tuweke kipaumbele cha juu katika kulinda Afya zetu kwani AFYA NI MTAJI; AFYA NI UTAJIRI. Pigania utajiri wa Afya then ndio upiganie utajiri wa mali.

Hivi sasa, nchi yetu inakabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu wenye MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA (MYA) kwa kizungu “Non Communicable Diseases (NCDs)”.

Magonjwa haya sasa yameongezeka kwa mara 5 hadi 9 zaidi kati ya miaka ya 80 na sasa. Miaka ya 80 ni asilimia moja (1%) tu ya Watanzania walikua na tatizo la Kisukari na asilimia 5 (5%) tu ndio walikua na tatizo la Shinikizo la Juu la Damu.

Hivi sasa watu wenye kisukari nchini ni asilimia 9 (9%) na Shinikizo la Damu ni asilimia 25 (25%)! Magonjwa haya yanatumia gharama kubwa kuyatibu sambamba pia na kusababisha ulemavu wa kudumu na vifo. Katika kila vifo 3 nchini, kifo kimoja kinasababishwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Magonjwa haya ni pamoja na:-
1. Shinikizo la Juu la Damu
2. Kisukari
Shinikizo la juu la Damu na Kisukari ndio kwa zaidi ya asilimia 70 husababisha mtu kupata magonjwa mengine yasiyoambukiza ambayo ni;-

3. Ugonjwa wa Moyo
4. Ugonjwa sugu ya figo (chronic kidney disease) na
5. Kiharusi (stroke)

Magonjwa mengine yasiyoambukiza ni;-
6. Saratani
7. Sikoseli
8. Magonjwa ya Afya ya akili

Unaweza kuzuia kupata magonjwa yasiyoambukiza. Vilevile endapo umeshapata magonjwa haya unaweza kuyadhibiti na kuishi maisha bora.

Mambo makubwa ya kuzingatia ili Kuzuia na Kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na;-

1. Kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa ikiwemo kula mbogamboga na matunda kwa wingi; kupunguza matumizi ya sukari, chumvi na mafuta mengi.

2. Kufanya mazoezi ya mwili au kuushughulisha mwili angalau mara 3 kwa wiki kwa muda usiopungua dakika 30. Hata hivyo wataalam wanashauri ili kupata matokeo mazuri zaidi muda ya mazoezi uwe angalau dakika 150 kwa wiki yaani dakika 30 mara 5 kwa wiki; au dakika 40 mara 4 kwa wiki au dakika 50 mara 3 kwa wiki.

3. Punguza unywaji wa Pombe kupita kiasi.

Mwisho, nisisitize wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara hasa kupima Shinikizo la Damu, Sukari pamoja na Uzito. Aidha ninawahimiza wananchi kupima saratani ikiwemo saratani ya matiti, saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya tezi dume. Ugonjwa ukigundulika mapema ni rahisi kuutibu.

#MtuNiAfya #JuaNambaZako #KingaNiBorakulikoTiba #NasahaZaOdoUmmy

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.