Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kuboresha huduma za Afya ya Kinywa na Meno nchini Tanzania kwa kutumia Tekinolojia mpya ya 3D Printing

Leo Oktoba 27, 2023 Waziri wa Afya Mhe. Ummymwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Ugeni kutoka Mashirika ya MCW Global ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Kinywa na Meno wa Shirika hilo Dkt. Marion Bergman  kutoka nchini Marekani akiwa ameambatana na  Shirika la Miracle Corners Tanzania ikiongozwa na Dkt. Katanta Simwanza.

Ajenda mbalimbali zimejadiliwa katika kikao hicho ikiwemo suala la namna ya kuboresha huduma za Afya ya Kinywa na Meno nchini Tanzania kwa kutumia Tekinolojia mpya ya 3D Printing ambayo inatumika kutengeneza vifaa visaidizi vya masuala ya Afya ya Kinywa na Meno.

Katika kikao hicho Waziri Ummy ameitaka timu yake kukaa pamoja na wadau hao kupitia Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) pamoja na Mkurugunzi Msaidizi wa idara ya Afya ya Kinywa na Meno ili kutengeneza mpango wa pamoja wa utekelezaji wa mradi huo uanze kutumika nchini Tanzania kupitia Tekinolojia hiyo.

Tekinolojia hiyo imebuniwa na Shirika la Sprintray yenye makao makuu yake nchini Marekani katika jimbo Calfonia ambao ni wataalamu wa tekinolojia ya  kutumia akili bandia (Artificial Inteligence).

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.