Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kutoa sumu mwilini,Fahamu Ukweli wa mambo

Kutoa sumu mwilini,Fahamu Ukweli wa mambo

Kutoa sumu mwilini: Ukweli nyuma ya hili ukoje? – Miaka ya hivi karibuni, dhana ya kwamba unahitaji kujisafisha ili kutoa sumu mwilini imepata umaarufu mkubwa. Mara nyingi imekua ikiambatana na bidhaa mbalimbali, milo ya kufanya diet na juisi mbalimbali zikitoa ahadi kuwa zitasafisha na kuondoa sumu mwilini. Lakini, ukweli ni kuwa, dhana ya kuwa unahitaji kujisafisha na kuondoa sumu mwilini mara kwa mara si kweli. Ni ulaghai unaotumiwa na watu wengi ili kujipatia pesa. Hebu tuangalie sayansi inasemaje?

Miili yetu imeundwa vizuri na ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu kwa njia ya asili kupitia viungo kama ini, figo, na mfumo wa kumeng’enya chakula. Viungo hivi vinafanya kazi bila kuchoka kutoa taka mwili nje na kudhibiti uwiano wa vitu mbalimbali mwilini.

Kunywa maji ya kutosha, kula mlo kamili na kufanya mazoezi ni muhimu katika kuusaidia mwili wako kutoa sumu zilizomo mwilini kwa njia ya asili.

Ni muhimu kutambua kuwa, hakuna utafiti wowote wa kisayansi unaothibitisha ufanisi wa bidhaa nyingi zinazosemekeana kuwa zinatoa sumu mwilini. Na ukweli ni kwamba, baadhi ya bidhaa za kujisafisha au kuondoa sumu au baadhi ya diet zinaweza kusababisha matatizo mwilini, zinaweza kusababisha ukakosa baadhi ya virutubisho mwilini, mvurugiko wa madini na chumvichumvi za mwili na hata kuvuruga utendaji kazi wa mifumo ya mwili.

Kama una wasiwasi kuhusu afya yako au kama unadhani unahitaji kuondoa sumu mwilini, ni vizuri kuonana na daktari  atakupatia ushauri wa kipekee unao kufaa wewe pekee kufuatia historia yako ya kimatibabu.



Badala ya kutegemea kutumia bidhaa maarufu za kuondoa sumu, ni vizuri kuzingatia kuwa na mfumo bora wa Maisha. Hii ni Pamoja na kula mlo kamili wenye matunda, mbogamboga, nafaka zisizokobolewa, na protini, kunywa maji ya kutosha, fanya mazoezi mara kwa mara na dhibiti msongo wa mawazo. Kuzingatia mambo haya, kutasaidia mwili wako kuondoa sumu yoyote ilimo kwa njia ya asili.

Kwa kumalizia, dhana ya kuwa unahitaji kusafisha au kuondoa sumu mwilini mara kwa mara si ukweli. Miili yetu imetengenezwa na uwezo mkubwa wa kuondoa sumu zote ka njia ya asili kupitia kwenye ini, figo na mfumo wa chakula. Usiende kutumia bidhaa zinazosababisha uhare, utapike au utokwe jasho kwa jina tu la kutoa sumu mwilini. Mtu yeyote anayekuambia hili ni tapeli na unapaswa kumkimbia. Kula vizuri, kunywa maji na kufanya mazoezi kutausaidia mwili kuondoa sumu vizuri kwa njia asili.

Chanzo: Healthline

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.