Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mapacha wawili Wafariki kwa Kuongezewa Matiti na Mganga wa Kienyeji ili waweze kuolewa

Watoto wawili ambao ni Mapacha wenye umri wa miaka 17 Wakazi wa Kijiji cha Bubale kilichopo Kata ya Nkololo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wamefariki dunia baada ya kupewa dawa na mganga wa tiba asili kwa lengo la kuwaongezea matiti ili waweze kuolewa.

Majirani waishio karibu na mganga huyo akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Byuna wamessma mganga huyo anaitwa Masunga Tumolo na wamekiri kuw Watoto hao walikuwa kwa mganga huyo Kijiji cha Byuna ambako walikwenda kuoga dawa ya kuwaotesha matiti.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Byuna, Dkt. Deogratius Mtaki amesema awali alipokea mwili wa Dotto na baadae akampokea Kulwa akiwa mahututi baada ya muda mfupi naye akapoteza uhai.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga @official_simalengatz amefika eneo la tukio ambapo amekemea kitendo hicho na kulitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na tukio la mauaji ya Mabinti hao.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.