Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mgomo nchi nzima Jumapili, huko Bangladesh kutoka chama kikuu cha Upinzani

Mgomo nchi nzima Jumapili, huko Bangladesh kutoka chama kikuu cha upinzani

Chama kikuu cha upinzani nchini Bangladesh kimeitisha mgomo wa nchi nzima kesho Jumapili baada maandamano iliyoyaitisha leo kumtaka waziri mkuu wa nchhi hiyo kujiuzulu kusambaratika.

Maandamano ya leo yalisambaratika kufuatia makabaliano makali baina ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa usalama. Polisi mmoja amekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mapambano yaliyotokea kati

kati mwa mji mkuu wa nchi hiyo Dhaka pale wafuasi wa upinzani walipoitikia wito wa kuandamana kumshinikiza Waziri Mkuu Sheikh Hasina kuachia madaraka kuelekea uchaguzi unaokuja.

Katibu Mkuu wa chama cha Bangladesh Nationalist  (BNP), ametoa mwito wa mgomo wa nchi nzima kesho ikiwa ni mwendelezo la shinikizo kwa Bibi Hasina aridhie kujiuzulu kupisha maandalizi ya uchaguzi.

Upinzani unataka kuundwe serikali ya mpito isiyoegemea upande wowote wa vyama itakayokuwa na dhima ya kusimamia uchaguzi unaokuja wa mnamo mwezi Januari ili kuufanya uwe huru na wa haki.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.