Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

NASA Kujenga nyumba Mwezini

Moja ya habari kubwa iliyotufungulia mwezi huu wa October ni kutoka Shirika la anga ya juu la Marekani la (NASA) ambalo limetangaza mpango wa ziara nyingine ya kudumu kuelekea kwenye mwezi huku likisema safari hii ya kipekee ni mwanzo kuelekea mpango wa kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2040, Wamarekani waanze kuishi kwenye nyumba zitakazojengwa mwezini.

Gazeti la The New York Times limeripoti kuwa baadhi ya Wanasayansi wanatilia shaka kwamba hatua hiyo inaweza ikawa ni ndoto tu ila Wanasayansi wa NASA wanasisitiza kwamba lengo la ujenzi wa nyumba kwenye mwezi mwaka 2040 linaweza kufikiwa kabisa.

“Tuko katika wakati muhimu na kwa kiasi fulani inaweza kuonekana kama ni ndoto, tukiangalia kwa upande mwingine, inaonekana kama hili ni jambo ambalo hatuwezi kulikwepa”

Ili kutekeleza ujenzi huo wa nyumna mwezini, NASA itatuma kifaa chenye uwezo wa kutengeneza michoro ya 3-D kuelekeza kwenye mwezi kisha kuanza kujenga miundo ya nyumba kwa kutumia mchanga, mawe na vipande vya madini vinavyopatikana kwenye pembezoni mwa volkano iliyoko kwenye mwezi ili kutengeneza nyenzo inayofanana na zege.

Nyumba hizo zitastahimili mabadiliko makubwa ya joto ya mwezi, mchanganyiko wa sumu ya meteorite na miale ya mwanga, hatua hii inajiri ikiwa imepita zaidi ya miaka 50 baada ya Mwanaanga Neil Armstrong kuwa Mtu wa kwanza kutembea juu ya mwezi kama sehemu ya kazi ya Apollo 11.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.