Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Sasa tumemaliza kazi ya aina za kisasa za silaha:Vladimir Putin

“Sasa tumemaliza kazi ya aina za kisasa za silaha za kimkakati ambazo nimezizungumzia na nilitangaza miaka michache iliyopita,”

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa nchi yake imefanya “jaribio la mwisho lililofanikiwa” la kombora la nyuklia.

“Jaribio la mwisho lililofanikiwa limefanyika Burevestnik na ni kombora la kimataifa linalotumia nguvu za nyuklia.”

Kombora hilo, lililopewa jina la Skyfall na muungano wa Nato, linasemekana kuendeshwa na kinu cha nyuklia, ambacho kinatakiwa kuwashwa baada ya kurushwa angani na roketi za mafuta.

Lakini gazeti la New York Times lilinukuu kundi la kampeni ya kudhibiti silaha za nyuklia , Nuclear Threat Initiative, likisema kwamba majaribio 13 ya awali ya mfumo huo kati ya 2017 na 2019 yote hayakufaulu.

Bw Putin pia aliwaambia wasikilizaji wake kwamba kazi ilikuwa karibu kukamilika kwa kombora lingine la masafa marefu, linaloitwa Sarmat.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.