Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Tujilinde, ukimwi bado unaua,Dkt. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuchukua tahadhari na kujilinda na maambukizi ya UKIMWI kwakuwa bado ugonjwa huo upo na unaua.

Rais Samia ameyasema hayo aliposhiriki kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mkoani Manyara ambapo pamoja na mambo mengine amewataka watanzania kujilinda na ugonjwa wa virusi vya Ukimwi kwani takwimu zinaonesha kwa mwaka watu elfu 29 wanafariki kutokana na ugonjwa huo.

“Nawaasa Watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya UKIMWI, pamoja na kwamba gonjwa hili sio janga tena , kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2020/2021 wastani wa Watanzania elfu 54 wanapata maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa mwaka na idadi ya vifo vinavyotokana na UKIMWI kwa mwaka ni takribani Watu elfu 29 sasa hii sio idadi ndogo, sio kama tulikotoka lakini hapa tulipofika hapajiridhisha niombe kila mmona ajilinde na janga hili” amesema Rais Samia.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.