Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Tuko pamoja Mhe:Rais Usitie mashaka kufanya Uwekezaji wa sekta ya Afya

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanlaus Nyongo amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwekeza katika sekta ya afya kwani wao kama wabunge wako bega kwa bega katika uwekezaji unaofanya na serikali.

Mhe. Nyongo amebainisha hayo katika uzinduzi wa ripoti ya tafiti ya afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria ya Mwaka 2022 halfa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

“tuko na wewe, watanzania wako na wewe usisite kufanya, unafanya kazi kubwa na sisi kama wabunge tuko na wewe katika uwekezaji wa sekta ya afya”. Mhe. Nyongo

Aidha Mhe. Nyongo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeboresha kwa kiwango kikubwa huduma za afya nchini kuanzia ngazi ya taifa mpaka kituo cha afya.

Pia, Mhe. Nyongo amesema maboresho katika sekta ya afya yamewezesha raia wa kigeni kuingia nchini kwa ajili ya kufata huduma za kibingwa na kibingwa bobezi kutokana na uwekezaji mkubwa wa fedha katika kuboresha huduma za afya

“Mhe. Rais umewekeza fedha nyingi katika kuboresha huduma za Kibingwa na bobezi nchini, sasa raia wa kigeni wanakuja nchini kupata huduma hizo. Pale JKCI kwa mwaka huu tumepata wageni kutoka nje ya nchi takriban 1500 waliokuja kupata matibabu”. Stanslaus Nyongo

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.