Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike kutoka kwenye korodani ya Mgonjwa wa jinsia mbili

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imefanikiwa kufanya upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike kutoka kwenye korodani ya mgonjwa wa jinsia mbili mwenye muonekano wa jinsia ya kiume,

upasuaji huo umefaywa na jopo la Madaktari kutoka Hospitali hiyo na limeongozwa na Daktari Bingwa wa upasuaji wa jumla na mfumo wa mkojo,

Dr Hussein Msuma pamoja na Wasidizi wake ,Dr Hamis Mbarouk,Mr Curtius Mbalamula, Mr Mkati na Sr Shani Maupa.

Upasuaji huo umefanyika kwa mara ya kwanza katika Hospitali hiyo na kwa mara ya kwanza kwa Hospitali za rufaa zilizopo Tanzania “Kufanyika kwa upasuaji huu ni moja ya mafanikio makubwa katika Sekta ya Afya Tanzania,

kwakuwa moja ya jitihada ya Serikali na wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha Hospitali zetu za Tanzania zinauwezo wa kutoa matibabu ya kibingwa na bingwa bobezi”

Akiongea baada ya upasuaji kufanyika na kufanya vipimo vya sampuli zilizotolewa katika upasuaji,

Dr Hussen Msuma amesema Mgonjwa mwenye umri wa miaka 22 alifika Hospitalini akiwa na muonekano wa jinsia ya kiume lakini ana maumbile ya ndani ya aina mbili yaani umbile la kike na la kiume,

hivyo kupelekea upasuaji huu “Upasuaji tumefanya kwa Mgonjwa aliyekuwa na muonekano wa nje wa jinsia ya kiume ila alikuwa na mifumo ya uzazi ya jinsia mbili, ya kiume kwenye korodani ya kulia na yakike kwenye korodani ya kushoto”

“Kwa lugha ya kitaalamu huu upasuaji unaitwa scrotal hystero-salpingo-oophorectomy na kwa lugha rahisi ni upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike kutoka kwenye korodani ya Mgonjwa wa jinsia mbili mwenye muonekano wa jinsia ya kiume,

ugonjwa huu unatokana na changamoto wa ukuaji wa kijinsia (ovotesticular DSD), ni ugonjwa nadra na adimu sana kutokea ambapo Mtu huzaliwa na viungo vya ndani vya uzazi (gonadi) za jinsia zote (ovari za kike na korodani za kiume), Mgonjwa kwa sasa anaendelea vizuri”

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.