Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Watoa huduma ngazi ya jamii kutambulika kimuundo

Watoa huduma ngazi ya jamii kutambulika kimuundo

Na WAF – Dodoma

Serikali imepanga kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo katika kuboresha huduma za afya kwa kuweka muundo utakaowatambua wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

Hayo yamebainika leo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma kilichowahusisha Viongozi wa Wizara ya Afya akiwepo Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu , Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na wawakilishi wa Mashirika na Taasisi za kimataifa zikiwemo WHO, USAID, UNICEF, AMREF, CDC, PEPFAR na wengineo.

Akiongoza kikao hicho Waziri Ummy amesema Ssrikali inaendelea kuboresha huduma za afya ngazi ya jamii hivyo wahudumu wamewekewa mkakati wa mafunzo maalum yatkayowasaidia kutoa huduma bora katika jamii inayowazunguka ikiwemo huduma za kinga.

Waziri Ummy amesema ili kufikia lengo hilo, Serikali haina budi kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo taasisi za kimataifa ili ziweze kufadhili mpango huo katika maeneo ambayo wataona yanafaa.

Wahudumu wa afya ngazi ya jamii ni wataalamu wa afya ambao hutoa huduma za msingi kwa jamii yao, kama vile elimu ya afya, kinga ya magonjwa, na matunzo ya kimsingi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.