Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Waziri wa Ufaransa alivyozomewa na Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Louis de Guiringaud alifanya ziara nchini Tanzania na ziara hiyo ikamtumbukia nyongo.

Wakati anatua alikutana na kundi kubwa la vijana zaidi ya 200, wanafunzi hawa wa UDSM wakiimba nyimbo za ukombozi na nyimbo za kuikashifu Ufaransa kwa kitendo chake cha kuiuzia silaha serikali ya kikaburu ya Afrika Kusini.

Hayati Benjamin Mkapa akiwa Waziri wa Mambo ya nje ndiye alikwenda kumpokea Louis de Guiringaud, Louis de Guiringaud alionesha kukasirishwa mno na vijana wale,

kwa dakika 10 palepale uwanjani alionekana akijibizana na Mh. Mkapa, na kutishia kusitisha ziara yake mara moja endapo vijana wale wataendelea kupiga kelele na kumzomea.

Baadae Louis de Guiringaud aligoma kabisa kufanya mkutano na Mh. Mkapa, na akamtuma msaidizi wake kwa Mkapa kwa sharti la aombwe msamaha kwa kudhalilishwa na Watanzania,

serikali ya Tanzania ikagoma kuomba msamaha na baada ya muda mchache, Louis de Guiringaud alipanda ndege yake na kuondoka.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.