Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Auliwa na Robot nchini Korea Kusini

Mwanaume mmoja nchini Korea Kusini amekutwa na mauti baada ya kukandamizwa na Roboti linalofanya kazi kwenye kiwanda cha kupakia mboga.

Polisi wameanza uchunguzi wa kisa hicho kubaini ikiwa roboti hilo halikuwa salama ama lilikuwa na hitilafu.

Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo alifariki kutokana na majeraha ya kichwani na kifuani, baada ya kushikwa na kukandamizwa kwenye mkanda wa kusafirisha mizigo na mikono ya roboti.

Kiwanda hicho kinatumia maroboti mawili kwa ajili ya kubeba mabox yaliyopakiwa mboga mboga za kusafirishwa nje ya nchi.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.