Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Breaking! matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2023 yametoka

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika September 2023,
ambapo Watahiniwa 1,092,960 sawa na asilimia 80.58 ya Watahiniwa 1,356,296 wenye matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2023 wamefaulu kwa kupata madaraja ya A,B na C.

Akitangaza matokeo hayo leo Jijini Dar es salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr.Said Mohamed amesema mwaka 2022 Watahiniwa waliofaulu walikuwa ni asilimia 79.62 hivyo ufaulu mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 0.96.

Wasichana waliofaulu ni 585,040 sawa na asilimia 80.58 ambapo ubora wa ufaulu umeongezeka ikilinganishwa na asilimia 78. 91 mwaka jana huku ubora wa ufaulu kwa Wavulana ukiongozeka ambapo waliofaulu ni 507,920 sawa na asilimia 80.59 ikilinganishwa na asilimia 80.41 kwa mwaka 2022.

“Katika ubora wa ufaulu Watahiniwa wengi wamepata daraja B na C ambapo daraja B ni Watahiniwa asilimia 23.20 daraja C ni asilimia 53.41 na daraja A ni asilimia 3.98”

Tazama Matokeo ya Darasa la Saba Hapa,2023;

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.