Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dakika 20 tu toka uache kuvuta Sigara mwili huanza kupata faida hizi

Angalia hii; ndani ya Dakika 20 tu baada ya kuacha kuvuta sigara, mwili wako huanza kupata faida.

Je wajua? ndani ya muda mfupi sana mwili wako huanza kupokea mabadiliko chanya toka uache kuvuta sigara?, Soma hapa

Dakika 20 tu toka uache kuvuta Sigara mwili huanza kupata faida hizi;

1. Baada ya dakika 20 toka uache kuvuta Sigara

  • Shinikizo la damu hushuka na kuwa kawaida
  • Mapigo ya moyo hushuka na kuwa kawaida
  • Mikono na miguu huwa na joto lake la kawaida

2. Baada ya saa 8, toka uache kuvuta Sigara,mabadiliko haya hutokea mwilini;

  • Kiwango cha Carbondioxide kwenye damu hurudi kawaida
  • Kiwango cha Oxygen kwenye damu hupanda juu

3. Baada ya saa 24, toka uache kuvuta Sigara,mabadiliko haya hutokea mwilini;

  • Hatari ya kupata tatizo la mshtuko au shambulio la moyo(Heart attack) hupungua

4. Baada ya saa 48, toka uache kuvuta Sigara,mabadiliko haya hutokea mwilini;

  • Mwili unakuwa huru kutoka kwenye Nicotine
  • Neva hurudi mahali pake na kuendana na mabadiliko ya mwili baada ya kuachana na nicotine
  • Hisia ya kujua Ladha pamoja na harufu ya kitu huanza kuwa bora zaidi(Sense of taste and smell improve)

5. Baada ya saa 72, toka uache kuvuta Sigara,mabadiliko haya hutokea mwilini;

  • Mirija kwenye mfumo wa hewa kwa kitaalam Bronchial tubes huanza kutanuka na kuruhusu hewa kupita vizuri
  • Mtu hupata urahisi wa kupumua vizuri

6. Baada ya wiki 2-13, toka uache kuvuta Sigara,mabadiliko haya hutokea mwilini;

  • Damu huzunguka vizuri zaidi,mzunguko wa damu huimarika zaidi
  • Ni rahisi hata kufanya mazoezi

7. Baada ya Mwaka 1, toka uache kuvuta Sigara,mabadiliko haya hutokea mwilini;

– Hatari ya kupata Magonjwa ya Moyo inapungua mpaka Nusu

8. Baada ya Miaka 5, toka uache kuvuta Sigara,mabadiliko haya hutokea mwilini;

– Hatari ya kupata Saratani ya Mlango wa kizazi kwa mvutaji wa Sigara huwa sawa na yule ambaye havuti Sigara.

– Hatari ya kupata Ugonjwa wa Kiharusi(Stroke) kwa mvutaji wa Sigara huwa sawa na yule ambaye havuti Sigara

– Hatari ya kupata Saratani ya Mdomo, Koo, Umio, na kibofu cha Mkojo hupungua kwa Nusu

9. Baada ya Miaka 10, toka uache kuvuta Sigara,mabadiliko haya hutokea mwilini;

✓ Hatari ya Kupata Saratani ya Mapafu(Lung Cancer) hupungua kwa Nusu.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.