Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Fahamu Zaidi kuhusu Saratani ya tumbo, Aina, Dalili, vipimo pamoja na matibabu yake

Saratani ya tumbo: ni saratani inayoanzia kwenye seli zinazozunguka tumbo. Tumbo ni kiungo kilicho upande wa kushoto wa sehemu ya juu ya fumbatio ambacho huyeyusha chakula. Njia ya usagaji chakula huchakata virutubishi katika vyakula vinavyoliwa na kusaidia kutoa taka kutoka kwenye mwili.

Mchakato wa usagaji chakula tumboni;

  • Chakula husogea kutoka kooni hadi tumboni kupitia mrija unaoitwa umio.
  • Baada ya chakula kuingia ndani ya tumbo, huvunjwa na misuli ya tumbo inayochanganya chakula na kioevu na juisi ya utumbo.
  • Baada ya kutoka tumboni, chakula kilichoyeyushwa kwa kiasi hupita kwenye utumbo mdogo na kisha huingia utumbo mkubwa.
  • Mwisho wa utumbo mpana, unaoitwa rektamu, huhifadhi taka kutoka kwa chakula kilichoyeyushwa hadi kitolewe nje ya njia ya haja kubwa wakati wa kutoa haja kubwa.

Aina za saratani ya tumbo

  • Adenocarcinoma.
  • Gastrointestinal stromal tumors (GIST).
  • Carcinoid tumors.
  • Lymphoma.

    Dalili za Saratani ya Tumbo

Huenda mwanzoni usione dalili zozote kwani wakati mwingine haioneshi dalili yoyote hadi isambae sehemu mbalimbali za mwili wako. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za ugonjwa wa saratani ya tumbo kama ifuatavyo:

  • Uchovu mwingi.
  • Kuhisi uvimbe au kushiba baada ya kula hata kama ni chakula kidogo tu.
  • Maumivu yaliyoambatana na kiungulia.
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Kuhara au kuvimbiwa
  • Maumivu ya tumbo
  • Kupungua kwa uzito bila sababu
  • Kutokuwa na njaa
  • Kinyesi cha damu au cheusi

VIPIMO:

Hivi ni Baadhi ya Vipimo ambavyo huweza kufanyika kwa Mgonjwa;

• Vipimo vya Damu(Blood tests)

• Kipimo cha endoscopy

• Ct Scan

• Ultrasound

• Kuchukua Kinyama na kwenda kukichunguza yaani Biopsy N.K

MATIBABU YA SARATANI YA TUMBO

Kama ilivyo kwa aina Zingine za Saratani, Kupata Tiba Mapema ndyo Kupona Kabsa, Lakini ukichelewa kupata Tiba na Saratani hii Kufikia Stage 4 ni ngumu zaidi kupata Tiba na Kupona,

Baadhi ya Matibabu yake ni Pamoja na;

– Mgonjwa kufanyiwa UPASUAJI

– Huduma ya chemotherapy

– Huduma ya radiation therapy

– Huduma Ya Chemo na Radiation kwa Pamoja yaani Chemoradiation n.k

kwa maelezo zaidi kuhusu saratani ya tumbo soma hapa

Saratani ya Tumbo,Chanzo,Dalili na Tiba yake

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.