Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Huduma ya upasuaji wa kurekebisha shape Mlonganzila kuanza rasmi Desemba mwaka huu

MKUU wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mlonganzila Dk Erick Muhumba amesema huduma ya upasuaji wa kurekebisha miili ya binadamu imepangwa kuanza Desemba mwaka huu.

Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Dar-es-salaam, Dk Muhumba amesema wamechelewa kuanza kwa huduma ya upasuaji ya kurekebisha miili ya binadamu ni kutokana na mtaalamu kutoka Afrika Kusini kuchelewa kufika nchini.

“Ni kweli tumechelewa kuanza upasuaji wa kurekebisha miili ya binadamu kwa sababu ya ukosefu wa vibali vya kumruhusu mtaalamu kutoka nchini Afrika ya Kusini kuja kufanya upasuaji huo” amesema Dk Muhumba

Amesema mtaalamu ambaye anakuja kufanya upasuaji wa kurekebisha miili anaitwa Dk Brian Monaisa ambaye ni Daktari bingwa wa upasuaji ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Chris Han Baragwanath iliyoko nchini Afrika ya Kusini.

Aidha Dk Erick amesema kutokana na ukosefu wa utaalamu huo, Idara ya Upasuaji wa Hospitali ya Muhimbili – Mlongazila imejipanga kutoa mafunzo kwa wataalamu wa ndani wa upasuaji ili baada ya miaka miwili basi upasuaji huo wa kurekebisha miili na upasuaji mwingine wa kupunguza uzito ufanywe na wataalamu bingwa wa ndani wa upasuaji.

“Tumejipanga kutoa mafunzo ya miaka miwili kwa wataalamu wa upasuaji wa kurekebisha miili ya binadamu na wale wengine wa kupunguza uzito basi watapatiwa mafunzo ya miezi sita,”.

Tangu kuanza kwa huduma ya upasuaji wa kupunguza uzito Hospitali ya Taifa ya Muhimbili – Mlonganzila imeweza kufanya upasuaji kwa watanzania wasiopungua 150 ambao wameweza kufaidika na huduma hiyo.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.