Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Husna Lucas alifungwa ‘plasta’ mdomoni akakosa hewa na hivyo kupoteza maisha

Mfanyakazi wa ndani Gilbert Mbumi, ameielezea Mahakama jinsi alivyoshuhudia mfanyakazi mwenzake Husna Lucas, akifungwa ‘plasta’ mdomoni jambo linalodaiwa kumsababisha kukosa hewa na hivyo kupoteza maisha.

Jambo hilo linadaiwa kufanyika wakati watu wanaodhaniwa kuwa majambazi walipovamia katika nyumba ya bosi wake iliyopo Mtaa wa Nkuruma, karibu na Mnara wa Askari, jijini Dar es Salaam.

Mbumi, mkazi wa Vingunguti, ametoa ushahidi wake leo Novemba 7, 2023 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbuni ambaye ni shahidi wa kwanza katika ya kesi ya mauaji inayowakabili washtakiwa watano, ametoa ushahidi wake mbele ya Jaji, Salma Magimbi.

Mbali na kutoa ushahidi wake, pia amewatambua washtakiwa watatu kati ya watano wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Husna Lucas.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Shabani Salum, Said Ramadhan, Riaz Abdul, Twaha Hassan na Iddi Rashid wanaodaiwa kutenda kosa hilo Desemba 27, 2021, Mtaa wa Nkuruma, karibu na mnara wa Askari, jiji hapa.

Siku hiyo ya tukio, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kumuua mwanamke aitwaye, Husna Lucas.

Akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Serikali Adolf Verandumi, shahidi huyo alidai anafanyakazi katika nyumba ya Abas Ismail iliyopo mtaa wa Nkuruma, karibu na Mnara wa Askari, miaka 30 sasa.

Alidai katika nyumba hiyo wapo wafanyakazi wawili, yeye na Husna Lucas ambapo Desemba 27, 2012 aliingia kazini saa 2 asubuhi.

Alidai, siku hiyo mke wa bosi wake aitwaye Masuma, alimkabidhi Sh30, 000 na kumweleza kuwa kuna mtu atapeleka mafuta ya kula hivyo amkabidhi fedha hizo za mafuta.

“Nilimuuliza huyo atakayeleta mafuta ni nani, akanijibu hamjui, atakayegonga mlango ndio huyo huyo, hivyo bosi wangu akaondoka na mumewe katika shuguli zao,” alidai Mbumi.

Alidai baada ya muda, mlango uligongwa na alipoenda kuchugulia katika kamera alikuwa mfanyakazi mwenzake Husna, akamfungulia mlango.

“Baada ya muda tena, mlango uligongwa nikachungulia katika kamera nilimuona mtu mwingine nikadhani ndio huyo ambaye bosi wangu aliniachia maagizo, hivyo nikafungua mlango,” alidai na kuongeza;

“Nilifungua mlango wa kwanza wa mbao, na kabla sijaimalizia kufungua wa pili, ulisukumwa kwa nguvu kwa ndani na kisha nikapigwa kabali, mtu mwingine alinipiga katika mbavu, nikaangushwa chini na kufungwa bandeji ya mdomo, na nikafungwa kamba za mikono na miguu,” alidai shahidi huyo.

Alidai akiwa hapo alisikia sauti ya Husna na baadaye haikusikia tena na kwamba watu hao walimpiga ngumi na mateke.

“Nakumbuka aliyenipiga kabali alivaa shati jeupe, mwingine alivaa ‘ovaroli’ rangi la bluu, niliyemuona katika kamera shati yenye maua ya njano ya mikono mirefu na kapelo ya bluu” alidai Mbumi.

Alidai, baada ya muda kulikuwa na ukimya hivyo alijivuta hadi eneo ambalo aliweza kuomba msaada kwa mlinzi ambaye alimfungua kamba na bandeji alizofungwa.

Alidai, Husna naye alikuwa amefungwa bandeji mdomoni na alikuwa hajiwezi hivyo, walipelekwa hospitali ya Hindu Mandal na baadaye Muhimbili kwa matibabu zaidi lakini baadaye alibaini Husna alifariki dunia.

Aliendelea kudai kuwa, Januari 24, 2022 aliitwa na askari mpelelezi kushiriki gwaride la utambuzi ambapo alifanikiwa kumtambua mshitakiwa Salum, Ramadan na Abdul.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.