Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Jaribio la sindano ya uzazi wa mpango kwa wanaume limefanikiwa

Hivi karibuni, jaribio lililofanywa na Baraza la Utafiti wa Matibabu la India (ICMR) limegonga vichwa vya habari katika ulimwengu wa matibabu.

Baada ya miaka saba ya utafiti, majaribio ya sindano ya uzazi wa mpango kwa wanaume yamekamilishwa kwa mafanikio.

Hii inamaanisha kuwa sindano hiyo sasa imeidhinishwa kwa matumizi.

ICMR imesema kuwa sindano hiyo haina madhara makubwa na ufanisi wake ni mkubwa.

Majaribio yanafanywa vipi?

Matokeo ya majaribio ya matatu ya dawa hiyo yalichapishwa mwezi uliopita katika jarida la Andrology.

Sindano hiyo, inayoitwa Reversible Inhibition of Sperm Under Guide (RISUG), ililazimika kupitia awamu tatu za upimaji kabla ya kupitishwa rasmi.

Watu kutoka Delhi, Udhampur, Ludhiana, Jaipur na Kharagpur walishirikishwa katika majaribio hayo.

Jaribio hilo liliwahusisha wanaume 303 wenye afya njema na wenye uhusiano wa kimapenzi wenye kati ya umri wa miaka 25 na 40 na wake zao.

Wanandoa hawa walijumuishwa katika jaribio tu wakati walipowasiliana na kliniki ya uzazi wa mpango.

Wanandoa hawa walikuwa familia ambazo zilihitaji kuvunga uzazi kwa njia ya vasectomy au kuamua kutokuwa na watoto zaidi.

Wakati wa majaribio haya, chini ya mwongozo, wanaume walipewa miligramu 60 . Dawa hii ilitolewa kwa wingi.

Via:Bbc

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.