Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kama wewe ni Mpenzi wa Viatu Virefu(high heels) tarajia kuona Matatizo haya

Kama wewe ni Mpenzi wa Viatu Virefu(high heels) tarajia kuona Matatizo haya

BAADHI YA MADHARA YA KUVAA VIATU VIREFU KWA WANAWAKE

(1) Kusababisha Maumivu ya mgongo na Kiuno

(2) Maumivu ya misuli ya nyuma ya miguu

maumivu ya misuli ya nyuma ya miguu; viatu virefu huleta maumivu makali ya misuli nyuma ya mguu kitaalamu kama calf muscles na ukiwachunguza vizuri watu wengi wanaovaa viatu hivyo hawawezi kusimama kwa muda mrefu yaani wataomba kiti wakae kila sehemu sababu ya maumivu makali, lakini pia mishipa huchomoza kwenye mishipa hiyo na kuleta maumivu inapoguswa.

(4) Kubadilika kwa muonekano wa Vidole

kubadilika kwa muonekano wa vidole; kutokana na kidole gumba kushindwa kuhimili mgandamizo unaopata kutoka kwenye mwili mzima, kidole hicho hujikuta kinapinda na kuleta shepu ambayo sio ya kawaida, hii sio nzuri sana kwa urembo na huweza kuleta maumivu.

mishipa ya damu kukunjika; mguu unaovishwa kiatu kirefu mara nyingi hujilazimisha kuingia kwenye kiatu kirefu na chembamba hii hufanya mishipa ya damu kujikunja sana na kua midogo sana na katika hali mbaya sana mishipa ya damu huweza kukatika.

(5) Maumivu ya joint ya mguu

presha kubwa kwenye joint ya mguu husababisha maumivu makali  ya joint hiyo na kuongeza hatari ya mtu kuvimba na kuumwa joint kitaalamu kama osteoarthritis.

(6) Kupinda kwa mgongo

kupinda kwa mgongo; kukosa kwa balance ya mwili wakati wa kutembea humfanya mtu kijaribu kupinda kidogo ili kupata balance, baada ya muda mrefu mgongo huanza kuzoea hali ile na kuleta maumivu makali yakiambatana na kupinda kwa eneo la juu na enoe la chini la mgongo.

(7) maumivu ya unyayo

katika matembezi ya kutumia viatu virefu kwa muda mrefu mgonjwa husikia maumivu makali ya kisigino, unyayo kwa chini na vidole kwa mbele, hii huweza kumnyima raha na kupunguza ufanisi wa shughuli zake za kila siku.

NB: Vaa viatu Virefu(high heels) kwenye matukio maalum, fashion shows n.k, ila Visiwe Viatu vyako vya Wakati Wote.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.