Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

kujisaidia makamasi, umekutwa na shida hii na unashangaa ni kwanini? soma hapa kufahamu

Je unajisaidia mafuta,damu au kamasi? unaweza kuwa na wasi wasi sana endapo hali ya kinyesi chako imebadilika na kuambatana na damu,makamasi au kuwa na vitu kama mafuta,

Katika makala hii tunachambua kuhusu tatizo la kujisaidia makamasi.

Sio kila wakati ukijisaidia kinyesi chenye kamasi ni tatizo, wakati mwingine ni hali ya kawaida. Kinyesi kwa kawaida kina kiwango kidogo cha kamasi ambacho husaidia kiweze kupita kirahisi kwenye utumbo mpana na kutoka nje.

Soma zaidi hapa kufahamu chanzo ikiwa ni tatizo, na je wakati gani hutakiwi kuogopa ikiwa umejisaidia kinyesi chenye makamasi,

Chanzo cha Kujisaidia Makamasi

Unaweza kujisaidia Choo chenye Makamasi kutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo;

1. Kuwa na Ugonjwa wa Amiba(amoeba),

DALILI ZA UGONJWA WA AMIBA NI PAMOJA NA;

– Mgonjwa kuanza kupata maumivu ya tumbo sana mithili ya tumbo kusokota

– Mgonjwa kuanza kujisaidia choo kilaini sana

– Wakati mwingine Mgonjwa kujisaidia kinyesi cha rangi ya kijani, kinyesi chenye vitu kama makamasi n.k

– Mgonjwa kuharisha au kujisaidia haja kubwa ya maji maji sanaa

– Mgonjwa kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu

– Mgonjwa kutoa hewa kwa njia ya haja kubwa mara kwa mara(kujamba)

– Mgonjwa kupata maumivu ya tumbo,Kifua na viungo mbali mbali vya mwili

– Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na Homa

– Mgonjwa kupatwa na tatizo la kupungukiwa na damu

– Kupoteza appetite ya chakula kabsa

– Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika

– Mgonjwa kupungua uzito wa mwili na kukonda

KUMBUKA; Moja ya njia ya mtu kupata vimelea hivi vya amoeba ambavyo husababisha ugonjwa huu wa amiba ni pamoja na kunywa maji machafu sana.

Maji ambayo yamechanganyika ma kinyesi cha mtu ambaye alikuwa na vimelea hivi vya amoeba.

SOMA ZAIDI Hapa kuhusu Ugonjwa huu wa Amiba

2. Maambukizi kwenye mfumo wa umeng’enyaji chakula

3. Ugonjwa wa crohns

4. Ugonjwa wa asaletive kolaitiz

5. Saratani ya utumbo mpana

6. Kuwa na shida ya mzio wa chakula n.k

Ni Wakati gani wa kuogopa unapojisaidia kinyeshi chenye makamasi?

Unapaswa kuwa na wasiwasi endapo kinyesi chenye kamasi kimekuwa na sifa zifuatazo;

  • Kamasi kuwa nyingi zaidi ya kawaida
  • Kamasi kuwa na michirizi au matone ya damu
  • Kimeambatana na mabadiliko ya tabia ya tumbo kama maumivu ya tumbo n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.