Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Madhara ya kunywa Pombe kwa Mgonjwa wa Sukari

Ugonjwa wa kisukari ni moja kati ya magonjwa mengi yasiyoambukiza (non-communicable diseases) ambayo yanongezeka kwa kasi na kusababisha vifo na ulemavu.

Taarifa ya International Diabetes Federation imesema watu millioni 463 duniani wanaishi na kisukari na millioni 19 ya hao wapo bara la Afrika pekee.

Shirika hili katika taarifa yake ya mwaka 2020 limesema kwamba uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari  nchini Tanzania ni kwa asilimia 3.7 huku idadi ya wagonjwa wa kisukari watu wazima imefika takribani watu 997,400.

Unywaji wa pombe uliopitiliza kwa watu wenye kisukari husababisha madhara makubwa ikiwemo kuongeza hatari ya kupata shinikizo la damu, magonjwa ya moyo,macho na kuharibika kwa mishipa ya fahamu.

Aidha Pombe au vileo vingi vina idadi kubwa ya wanga na sukari hivyo husababisha kupanda kwa haraka kwa sukari kwenye damu. Pia vina kalori nyingi hii upelekea kuwepo hatari ya kuongezeka uzito uliopitiliza ambapo hupunguza unyeti (sensitivity) na utolewaji wa kichocheo aina ya insulin  mwishowe husababisha ugumu wa kudhibiti sukari yako mwilini.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.