Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

“Magufuli nakuahidi kama unaweza kusikia,nitakuwa msema kweli” Paul Makonda

GEITA; Chato. Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Ziwa, leo amefika nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, hayati Dk John Pombe Magufuli wilayani Chato mkoani Geita na kuzuru kwenye kaburi lake.

Makonda ameongoza sala fupi na kusema: “Magufuli nakuahidi kama unaweza kusikia, Rais Samia Suluhu Hassan amenipa nafasi, nitakuwa msema kweli, nitakuwa mwaminifu kwa taifa langu na chama changu, na wewe huko uliko uendelee kuniombea ya kwamba ile kazi njema uliyotamani ifanyike katika taifa hili chini ya jemedari na kiongozi uliyemuachia nitakuwa sehemu ya kumsaidia na kumtia moyo Rais wangu Samia.

“Na kupitia yeye naamini Taifa litanufaika zaidi, asante kwas ababu ulilipenda Taifa hili nasi tunakuahidi upendo huo, ulishatuambukiza kwetu, tutaendelea kuwa wazalendo na tutalilinda taifa hili na siku moja tukitwaliwa na sisi tukaache alama kama Magufuli ulivyoacha alama katika Taifa hili la Tanzania,” aliomba Makonda.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.