Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Msitumie Biskuti msizozifahamu kwani nyingi zimekuwa zikichanganywa na dawa za kulevyia

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya imefanikiwa kukamata Madawa ya kuleva aina ya Bangi yenye sumu Kali maarufu kama Skanka yenye uzito wa Kg 423 nchini ambapo Kg 158 zimekamatwa kwenye fukwe za Bahari ya Hindi maeneo ya Kawe pamoja na Kigamboni.

Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Aretas Lyimo wakati anatoa taarifa ya oparesheni ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanaziba mianya ya Dawa za kulevyia nchini.

Aidha mamlaka hiyo inasema watuhumiwa 16 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini kwa tuhuma za kumiliki kiwanda cha kutengeneza Biskuti zinazochanganywa na Skanka, ambapo watuhumiwa 6 wameshafikishwa Mahakamani na wengine 10 watafikishwa baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Aidha Kamishna ametoa wito kwa watoto pamoja na wanafunzi kutotumia Biskuti ambazo hawazifahamu kwani nyingi zimekuwa zikichanganywa na madawa ya kulevya hali inayopelekea kuhatarisha maisha yao kutokana na madawa hayo yamekuwa na sumu kwa kiwango kikubwa kinachoweza kuamsha wagonjwa ya afya ya akili na kupelekea kufanya vitu hatarishi

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.