News
Serikali imekubali kulipa Shilingi Bilioni 228 za NHIF
Kuhusu deni la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) linaloidai Serikali Waziri @ummymwalimu amesema Serikali imekubali kulipa Shilingi Bilioni 228 za NHIF,
ambazo ni deni la Wizara ya Mambo ya Ndani Tsh. Bilioni 45.4, Taasisi ya Mifupa (MOI) Tsh. Bilioni 18.2, NIDA Tsh. Bilioni 17.3 na Hospitali ya Benjamin Mkapa Tsh. Bilioni 129.
Madeni haya yatalipwa ili kulinda uhai na uendelevu wa Mfuko. Mhe. Ummy ameyasema haya Bungeni wakati akijibu hoja za ripoti ya CAG ya mwaka 2021/2022.