Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Shabiki wa Yanga Apigwa na rungu kisha kufariki kwenye Duka lake mwenyewe akizaniwa Mwizi

Walinzi watatu wa Kampuni ya Samike Security Campany iliyopo Wilayani Geita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za Kumpiga rungu na kumuua Mfanyabiashara na Shabiki maarufu wa Yanga Alex Mayaya (40) baada ya kumhisi ni Mwizi usiku wa November 05,2023.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku akisema chanzo ni Walinzi hao kujichukulia sheria mkononi.

“Baada ya ushindi ule wa Yanga, Alex alishangilia kupita kiasi na akanywa pombe za kupita kiasi kisha akaenda kwenye duka lake lililopo eneo la Kilimahewa Katoro Wilaya ya Geita na akafungua hilo duka na akatoa matairi mawili ya pikipiki huyo Mfanyabiashara alikuwa anauza vifaa vya pikipiki, kwa bahati mbaya duka lake lile linaendeshwa na Kijana wake kwahiyo wale Walinzi hawamfahamu vizuri wakahisi ni Mwizi kwahiyo baada ya kuhisi ni Mwizi walimkamata walimshambulia kwa kumpiga na rungu”

“Baada ya kumpa kipigo Mfanyabiashara huyo Walinzi hawakumpeleka Kituo cha Polisi walikaa nae mpaka asubuhi kulipokucha huku hali yake ikiwa mbaya na kupelekea umauti wake baada ya kumfikisha Hospitali kwa matibabu zaidi asubuhi”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.