Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

TMDA wasimamie Maduka ya Dawa,Usugu wa vimelea dhidi ya dawa mwilini (Antimicrobial resistance AMR) ni tishio kubwa

Ongezeko la matumizi holela ya Dawa za Antibiotiki

Na. WAF – Dodoma

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa mwilini (Antimicrobial resistance AMR) ni tishio kubwa la afya kwa jamii ya Watanzania hivyo Serikali imeweka mikakati madhubuti ili kukabiliana na tatizo hilo kwa kuimarisha udhibiti kwa kuanza mchakato wa kuondoa usimamizi wa maduka ya Dawa kutoka Baraza la Famasi na kupeleka majukumu haya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)

Waziri @ummymwalimu amebainisha hayo kwenye ukurasa wake wa mtandao X wakati akijibu hoja ya Frank Arabi alipohoji kuhusu matumizi sahihi ya dawa za antibiotiki.

Waziri Ummy amesema kumekuwepo na matumizi yasiyo sahihi ya dawa nchini na hivyo kufanya dawa nyingi za Antibiotiki hivyo kuwa na ufanisi mdogo katika kutibu magonjwa.

“Pamoja na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya dawa za Antibiotiki, tatizo hii kwa kiasi kikubwa linachochewa na  baadhi ya wataalam wetu kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya taaluma”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amewataka wahudumu wa Afya hasa Madaktari na Wafamasia kusimamia jukumu hilo ili Watanzania wapate uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.