Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Unakutana na mtu Amevaa Vizuuri Kumbe ni Mwizi: Mbunge wa Geita vijijini

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma amesema hali iliyofikia sasa ni mbaya kiasi kwamba mtu anajifanya ni mwema, anavaa vizuri kumbe anaiibia Serikali.

Musukuma amewaomba Wabunge waisaidie Serikali, kwani inaibiwa sana na fedha iliyotajwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) sio ndogo ambayo ingesaidia kwenye miradi mbalimbali.

“Tuna maamuzi kabisa kama Bunge, sheria inaturuhusu kuchukua maamuzi kuielekeza Serikali na msipotusikiliza basi tuchukue maamuzi kwenu wenzetu ambao tumewatuma kwenda kutuwakilisha huko kwenye Serikali, kwa kweli pesa zinaibiwa mno yani unafika mahala mimi najiuliza elimu yangu ni ndogo lakini nikijiuliza hivi maana ya shule ni wizi au ni kitu gani maana mnasumbua sana wasomi”. amesema Musukuma

Amesema wao kama Wabunge wanatimiza wajibu wao wa kuwaeleza Mawaziri ubadhirifu unaofanyika kwenye halmashauri zao lakini mchakato wa kuchukua hatua unakaa muda mrefu.

“Najiuliza kitu kidogo wafanyabishara ukikosea tu kitu kidogo TRA hao, funga akaunti chukua hela nyinyi mnaotuibia matrilioni kwa nini mko nje na mimi sitaki kwenda hata mbali kusema kunyonga, tufungue magereza tunayo mashamba makubwa ya NARCO chukua peleka gereza la kilimo wapeleke walime mpaka warudishe zile hela”. amesisitiza Musukuma

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.