Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Ajira 500 za wauguzi wa kike kuajiriwa Nje ya Nchi, Serikali ya Saudi Arabia

Ajira 500 za wauguzi wa kike kuajiriwa Nje ya Nchi, Serikali ya Saudi Arabia

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemej akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, leo Desemba 18 2023.

Mhandisi Luhemeja amshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake kuhakikisha watanzania wananufaika na ajira

Na MWANDISHI WETU

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza neema ya uwepo wa ajira 500 za wauguzi wa kike kuajiriwa na Serikali ya Saudi Arabia mapema mwezi Januari 2024.

Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, leo Desemba 18 2023, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na dhamira yake thabiti ya kuhakikisha watanzania wananufaika na fursa za ajira zinazojitokeza kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na mataifa mbalimbali duniani.

Mhandisi Luhemeja alisema hivi karibuni mwishoni mwa mwezi Novemba na mwanzoni mwa mwezi Desemba, 2023, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya kazi na ajira na Serikali ya Saudi Arabia pamoja na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Alisema hati za mashirikiano zilizosainiwa zinatoa fursa za ajira kwenye mataifa husika kwa kada na sekta zenye kutumia ujuzi wa chini, ujuzi wa kati na ujuzi wa juu.

“Hati hizo zinalenga kuongeza fursa za ajira kwa watanzania kwenye nchi husika na pia kuweka utaratibu rasmi wa kuratibu ajira za watanzania wanaoenda kufanya kazi nje, ili kuhakikisha wajibu na haki za watanzania husika zinalindwa na kuzingatiwa ipasavyo,” alisema Mhandisai Luhemeja.

Alisema watanzania wote wenye sifa na ujuzi uliobainishwa wanataarifiwa kuomba kazi husika kwa kujisajili https://jobs.kazi.go.tz na kutuma wasifu binafsi ((CV) kwa njia ya barua pepe esu@taesa.go.tz, ambapo mnwisho wa kutuma maombi ni tarehe 27 Desemba 2024.

Mhandisi Luhemeja alisema kwa watanzania ambao tayari wamejiandikisha wawasilishe wasifu binafsi (CV) zilizohuishwa kwa njia ya barua pepe esu@taesa.go.tz.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Luhemeja alisema Serikali inaendelea kufanya mashauriano katika hatua mbalimbali na nchi zingine zaidi ya kumi (10) kwa lengo la kuwa na makubaliano ya ushirikiano utakaowezesha watanzania kunufaika na fursa za ajira kwenye nchi husika.

“Tunampongeza sana Rais Samia kwa kuwa chachu ya kufanikiisha mazungumzo haya muhimu. Dhamira yetu ni kuhakikisha Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi zinazotoa nguvukazi shindani kufanya kazi sehemu mbalimbali duniani,” alisema Mhandisi Luhemeja.

Alitoa wito kwa watanzania wote wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo katika fani zote wenye nia ya kufanya kazi nje ya nchi kujisajili Kitengo cha Huduama za Ajira (TaESA) kupitia https://jobs.kazi.go.tz na kusisitiza kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu kupitia TaESA imejipanga kuendelea kutekeleza wajibu muhimu wa kusajili na kuwajengea uwezo watanzania wenye nia na shauku kwenda kufanya kazi nje ya nchi ili kumudu ushindani pamoja na kufanya kazi kwa tija.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.