Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Celine Dion ‘hana udhibiti tena wa misuli yake, chanzo ugonjwa wa stiff person syndrome

Celine Dion ‘hana udhibiti tena wa misuli yake, chanzo ugonjwa usiotibika wa stiff person syndrome.

Mwimbaji mashuhuri wa Kanada Celine Dion mwenye umri wa miaka 55, hana tena “udhibiti wa misuli yake,” kulingana na dadake mkubwa Claudette mwenye umri wa miaka 75,

Chanzo kikubwa ni yeye kuugua ugonjwa mbaya usiotibika unaofahamika kitaalam kama stiff person syndrome.

Desemba iliyopita, mwimbaji huyo aliahirisha ziara yake ya kwenda Maeneo mbali mbali Duniani na akatangaza kwamba ana ugonjwa wa neva unaoitwa stiff person syndrome.

Dada yake mkubwa amependekeza kuwa inaweza kuchua muda kabla ya Celine kurejea jukwaani.

Hali ya Celine, ambayo ni endelevu na isiyotibika, husababisha mwili kushambulia seli zake za neva na kuathiri sana uhamaji wake,kuathiri uwezo wa kudhibiti misuli ya mwili n.k

“Anafanya kazi kwa bidii, lakini hana udhibiti wa misuli yake. Kinachovunja moyo wangu ni kwamba amekuwa na nidhamu kila wakati,” Claudette aliambia 7 Jours.

“Daima amefanya kazi kwa bidii. Mama yetu kila mara alimwambia, ‘Utafanya vizuri, utafanya ipasavyo.’

Aliendelea: “Ni kweli katika ndoto zetu na zake, lengo ni kurejea jukwaani. Katika nafasi gani? Sijui.”

Claudette aliongeza: “Njia za sauti ni misuli, na moyo pia ni msuli. Hii ndio inakuja kunipata. Kwa sababu ni kisa 1 kati ya milioni, wanasayansi hawajafanya utafiti mwingi kwa sababu haukuathiri watu wengi hivyo.

Shirika la hisani la familia ya Celine, Fondation Maman Dion, limejawa na jumbe za kumuunga mkono nyota huyo.

Claudette alisema: “Watu wengine wamepoteza tumaini kwa sababu ni ugonjwa ambao haujulikani vizuri. Laiti ungejua idadi ya simu ambazo Foundation hupokea kuhusu Celine!

“Watu wanatuambia wanampenda na wanamuombea. Anapata jumbe nyingi, zawadi na misalaba yenye baraka.”

Claudette amefichua hapo awali kwamba licha ya kufanya kazi na “watafiti wakuu katika uwanja huo,” dada yake ameona uboreshaji mdogo katika afya yake.

Aliiambia Le Journal de Montreal: “Hatuwezi kupata dawa yoyote ambayo inafanya kazi, lakini kuwa na matumaini ni muhimu.”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.