Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Dalili za upungufu wa protini mwilini

Dalili za Upungufu wa Proteins mwilini

Virutubisho(nutrients) vya Proteins tunaweza kuvipata kwenye vyakula mbali mbali ikiwemo;

  • Nyama,
  • Samaki,
  • Mayai,
  • Maharage,
  • Kuku,
  • Maziwa n.k

endapo Mwili wako haupati Proteins za Kutosha,Utaanza kuona mabadiliko mbali mbali mwilini,

Na Hizi ni Dalili na Ishara Kwamba Mwili wako haupati PROTEINS za Kutosha;

1. Kuwa na tatizo la Misuli Kukosa Nguvu,

2. Kuvimba kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama vile;

  • Miguuni,
  • kwenye mikono,
  • Tumboni n.k

Japokuwa kuna vitu vingi huweza kusababisha tatizo hili la Kuvimba,Hivo ni vizuri kufanya vipimo Kwanza.

3. Kuwa kwenye hatari ya Kupatwa na shida ya Msongo wa Mawazo Zaidi au Kuwa aggresive zaidi(Mood changes),

Tafiti zinaonyesha,Ubongo wako hutumia kemikali ambazo hujilikana kama neurotransmitters,ambazo hupitisha Taarifa mbali mbali kwenye Seli,

Na asilimia kubwa ya Hizi neurotransmitters Zinatengenezwa na AMINO ACIDS(Proteins), Hivo Mwili kutokuwa na Virutubisho vya Proteins vya kutosha pia huweza kupelekea kiwango cha neurotransmitters kupungua sana,

Na hivo kuathiri kwa kiwango kikubwa utendaji kazi wa Ubongo,

Pamoja na kiwango kidogo cha dopamine na serotonin, unaweza kuwa na msongo zaidi wa mawazo au kuwa aggressive zaidi.

4. Madiliko kwenye Nywele,Kucha,Pamoja na Ngozi yako

Vitu vyote hivi vimetengenezwa au Nimatokeo ya Proteins kama vile elastin, collagen pamoja na keratin.

Kama mwili wako hautengenezi vitu hivi unaweza kuona matokeo mbali mbali ikiwemo;

• Nywele zako kuwa nyembamba zaidi(kukosa afya),kunyonyoka haraka,kutokuwa nyingi au kukuwa vizuri n.k

• Ngozi kubadilika na kuwa Kavu zaidi,kupasuka,kutoa magamba n.k

• Kucha kuwa na mikunjo zaidi au matuta ya kina,kutokuota vizuri n.k

5. Mwili kupata Uchovu sana na kuwa dhaifu, hii ni kutokana na Misuli ya mwili kuathiriwa(Loss Muscle mass)

6. Kuhisi njaa sana mara kwa Mara, tafiti zinaonyesha kula vyakula vya Proteins hukufanya ujihisi Umeshiba Muda wote,

Proteins ni Moja ya vyanzo vikubwa vitatu vya Calories, ikiwa ni Pamoja na Carbs na Fats.

Hivo bila shaka upungufu wa proteins utakufanya uhisi njaa kwa haraka zaidi.

7. Vidonda na Majeraha kuchelewa zaidi Kupona,

Haya huweza kutokea kwa sababu ya mwili wako Kutokutengeneza Collagen za kutosha,ambapo haya ni matokeo ya Upungufu wa Proteins Mwilini

8. Tatizo la Damu Kutokuganda,

Pia hata Swala la Damu kuganda huhitaji Uwepo wa Proteins pia.

9. Kuumwa au Kuugua Mara Kwa Mara, Hii ni kutokana na kuathiriwa kwa Mfumo wako wa Kinga Mwili,

Amino acids(Proteins) kwenye Damu husaidia mfumo wa Kinga ya Mwili kutengeneza antibodies ambazo huhamasisha seli nyeupe za Damu(white blood cells) kupambana na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; viruses, bacteria au hata Sumu mbali mbali(toxins),

Hivo bila shaka kuathiriwa kwa mfumo wa kinga Mwili,kutafanya iwe rahisi sana mwili wako kushambuliwa na magonjwa mbali mbali.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.