Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Faida za Maji ya Limao yaliyochemshwa

Faida za Maji ya Limao yaliyochemshwa

Maji ya limao yaliyochemshwa hutajwa mara nyingi kama tiba asilia ya magonjwa mbalimbali. Watu wengine wanadai kuwa inaweza kupunguza uzito, kusafisha ngozi yako, na kuongeza kinga ya mwili.

Kinywaji hiki cha maji ya limao hutengenezwa kwa kuchemsha ndimu,limao iliyokatwa au maganda ya limao kwenye maji. Katika baadhi ya matukio kulingana na anachotibu mtu kwa wakati huo basi unaweza kuongeza viungo vingine, kama vile tangawizi, sukari,asali, mdalasini, au pilipili.

Ingawa wengi huamini zaidi katika matumizi ya tiba hii ya asili, lakini pia wapo wengine wanaweza kujiuliza ikiwa kuna ukweli wowote kwenye tiba hii.

Zifuatazo ni Faida za Kiafya za Maji ya Limao yaliyochemshwa;

1.Kuzuia Mawe kwenye Figo

Utafiti unaonyesha kuwa maji ya limao yaliyochemshwa yanaweza kusaidia kuzuia mawe kwenye figo(calcium oxalate).

Kwani calcium oxalate huweza kuundwa kwenye figo na kusababisha maumivu makali ya figo na dalili zingine kama vile kichefuchefu na kutapika.

2. Kusaidia Kupunguza Uzito

Maji ya limao ya kuchemsha yanaweza kuwa chaguo nzuri na sahihi ikiwa unatafuta kupunguza uzito. Hata hivyo, hiyo inawezekana kwa sababu maji husaidia kupunguza uzito.

3. Maji ya limao yanaweza kusaidia kuongeza kiwango cha Maji mwilini

Kuongeza maji ya limao yaliyochemshwa kwenye mlo wako ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa unakunywa maji ya kutosha siku nzima.

Maji ya limao yanaweza kuwa ya manufaa hasa kwa wale ambao hawapendi kunywa maji ya kawaida na badala yake wanapendelea vinywaji vyenye ladha.

Matumizi ya maji ni muhimu sana, pia yana faida nyingi za kiafya. Maji husaidia katika shughuli mbali mbali;

  • za kimetaboliki,
  • umeng’enyaji wa chakula,
  • utendaji kazi wa ubongo,
  • afya ya figo na mengine mengi.

Kinyume chake, upungufu wa maji mwilini unaweza kusababisha dalili nyingi zisizo nzuri ikiwa ni pamoja na kubanwa kwa misuli, maumivu ya kichwa, ngozi kuwa kavu na uchovu wa mwili.

Ikiwa unatumia vinywaji vyenye sukari mara kwa mara kama vile soda, chai, au vinywaji vya michezo vyenye sukari na unataka kuzuia unywaji wako,Basi maji ya limao yaliyochemshwa yanaweza kuwa mbadala mzuri.

Hitimisho:

Hizo ndyo baadhi ya Faida za Maji ya Limao yaliyochemshwa.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.