Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Makonda amchangia Professor Jay Million 20, Prof. Jay Foundation “peleka tabasamu na saidia Wagonjwa wa figo nchini”

Makonda amchangia Professor Jay Million 20, Prof. Jay Foundation “peleka tabasamu na saidia Wagonjwa wa figo nchini”.

Katibu wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda @baba_keagan , ametimiza ahadi yake ya kumchangia Tsh Milioni 10 aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi na Msanii Joseph Haule maarufu Professor Jay @professorjaytz .

Mwenezi Makonda ametimiza ahadi hiyo leo alipofika nyumbani kwa Professor Jay Jijini Dar es salaam ambapo pia amemkabidihi Professor Jay Tsh. milioni 10 nyingine ikiwa ni mchango kutoka kwa Ndugu wa Mwenezi Makonda na kupelekea kuwa amekabidhi jumla ya Tsh Milioni 20.

Akiongea na Makonda, Professor Jay amesema anapata changamoto ya umbali kutoka anapoishi sasa hadi kufika Hospitali ya Muhimbili ambapo Makonda amemuahidi kumtafutia nyumba na kumlipia eneo la Upanga ili kusudi kuepukana na changamoto hiyo anayoipitia.

Professor Jay pia ameelezea changamoto ya Watu walioahidi kuchangia kusuasua ambapo Makonda amemuahidi Professor Jay kumsaidia katika kuwakumbushia wale wote walioahidi kumchangia kukamilisha ahadi zao.

Ikumbuke kuwa Mwenezi Makonda alitoa ahadi yake binafsi kumchangia Professor Jay siku ya uzinduzi wa Prof. Jay Foundation ili kupeleka tabasamu na kusaidia Wagonjwa wa figo nchini.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.