Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mtoto kutoa povu mdomoni,chanzo chake ni nini?

Mtoto kutoa povu mdomoni,chanzo chake ni nini?

Kutoa Povu Mdomoni ni dalili za matatizo mbali mbali ikiwemo degedege,kifafa n.k

Kwa Ugonjwa wa Kifafa, Huu ni ugonjwa ambao wataalamu wanasema unatokana na hitilafu au jeraha katika ubongo
linalosababisha mgonjwa kuanguka,kukakamaa, kuzimia na wakati mwingine kutoa povu mdomoni.

Hali huwa ngumu zaidi pale
wagonjwa hao wanapoanguka; jamii inayowazunguka imekuwa ikishindwa kuwasaidia kwa wakati kwa kudhani ni mapepo, watu hawa wanahitaji msaada wa haraka hasa pale wanapodondoka chini.

Mtoto kutoa povu mdomoni

Moja ya sababu kubwa kwa Mtoto kutoa povu mdomoni ni pamoja na hii ya kuugua Degedege, Soma Zaidi hapa kuhusu degedege kwa Watoto.!!!!

Visababishi vya degedege kwa watoto ni pamoja na;

• Mtoto Kuwa na joto la kiwango cha juu (zaidi ya selsiasi 38)

• Pengine kama mtoto aliumia ubongo wakati akiwa bado tumboni

• Au kama alikosa oksijeni wakati mama anajifungua. Na hali hii inaweza baadaye kugeuka na kuwa kifafa.

• Mtoto Akipata maambukizi yakaingia kwenye ubongo,

• Mtoto kupata ajali.n.k

Dalili za Ugonjwa wa degedege kwa Watoto

Dalili za Ugonjwa wa degedege kwa watoto ni pamoja na hii;

1. Mtoto kutoa mate au hata povu mdomoni

2. Unaweza kumuona mtoto ametoa jicho anaangalia juu tu,

3. au ukaona shingo yake ni kama inageuka isivyo kawaida, kupinda upande mmoja n.k

4. Mtoto anaweza kukakamaa kabisa au akageuka tu upande mmoja na akasalia hivyo

5. Mtoto anaweza kupoteza fahamu kabisa

6. Mtoto kuwa na hisia za kupitiliza kama kucheza au kulia sana, furaha isiyo ya kawaida, hofu au hata uwoga

7. Mtu anaweza kuanza kuzungumza mambo yasiyoeleweka hata ukahisi kama akili yake imeanza kuwa na matatizo

8. Kuchezesha macho, kutoa mate au povu mdomoni

9. Misuli kukakamaa, inaishiwa na nguvu na kupelekea kuanguka

10. Lakini pia anaweza kutokewa na dalili zingine…!!!

Ukiona hali kama hii kwa Mtoto wako hakikisha anapata msaada wa matibabu kwa haraka Zaidi.

AU KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.