Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Afya ya mtoto mchanga wa siku 14 baada ya kukutwa kwenye pipa la maji

Afya ya mtoto mchanga wa siku 14 baada ya kukutwa kwenye pipa la maji

Singida. Mtoto mwenye umri wa siku 14 amekutwa amefariki dunia kwenye pipa la maji ambamo inadaiwa alitupwa na mama yake.

Tukio hilo limebainika asubuhi ya leo Januari 21, 2024 katika Mtaa wa Mwajakitope Manispaa ya Singida huku ndugu wa familia wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Si mara ya kwanza kwa matukio ya wazazi kuwaua watoto wao kutokana na sababu mbalimbali, matukio kama hayo yamekuwa yakiripotiwa na vyombo vya dola kuanza.

Katika tukio la Januari 12, 2024, mtoto wa miezi mitano, Leornad Kabilu alikufa huko Geita baada ya kupigwa na baba yake sehemu mbalimbali mwilini kwa kutumia mkanda na kiatu kwa kile kilichoelezwa na mama wa mtoto huyo, kwamba alikuwa analia wakati wamelala.

Tukio jingine la Januari 17, 2024, ni la kichanga cha kiume kilichokutwa kimetelekezwa jalalani bila nguo na mtu asiyejulikana katika Mtaa wa Kiyangu A, manispaa ya Mtwara Mikindani huku jeshi la polisi likiendelea kumsaka mhusika.

Akizungumza kichanga kilichokutwa kwenye pipa, baba mdogo wa binti anayedaiwa kuwa mzazi wa mtoto huyo, Ally Athumani amesema mama wa kichanga hicho alikuwa anasoma shule ya sekondari Mwankoko iliyopo mkoani Singida na aliacha shule mwaka uliopita na mwaka huu alitakiwa kuingia kidato cha pili.

Mwenyekiti wa mtaa huo, John Paskal amesema asubuhi alipigiwa simu akiambiwa mtoto amepotea katika mazingira yasiyoeleweka kisha akaongozana na majirani kumtafuta katika mashamba na baadaye katika mazingira ya nyumbani.

Amesema alipoingiza mti kwenye pipa lenye maji nje ya nyumba, kikatokea kichanga hicho.

“Nimepigiwa simu asubuhi na mwenye nyumba baada ya kufika hapa nikaelezwa kwamba kuna mtoto amezaliwa, ana siku 14 lakini mtoto amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, ikaonekana labda ni mambo ya uchawi lakini hayo maelezo hayakuingia akilini kwangu.

“Nikawaambia tutoke tutafute kwenye mashamba lakini baada ya kurudi nyumbani Mungu naye sijui alinigusa wapi, nikauliza hili pipa mbona lina maji wakasema ni ya kuoga. Nikaingiza fimbo nikakutana na kitu chini, baada ya kunyanyua ndipo akatokea mtoto,” amesema mwenyekiti huyo.

Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Singida, Ramadhani Ngoloma amesema mara baada ya kufika wamewachukua wahusika wa familia nzima kwa ajili ya mahojiano na mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi.

“Baada ya kupata hizo taarifa tumekuja, tumehoji na tumewachukua kwa ajili ya mahojiano zaidi ya kisheria,” amesema Ngoloma.

Amesema matukio ya namna hii yanatokana na malezi mabovu kwa watoto na jamii haiwajibiki ipasavyo na kusababisha watoto kuanzisha uhusiano wakiwa na umri mdogo.

Aika Jumanne, jirani na familia hiyo amesema ni bora mtoto huyo angepewa yeye amlee kuliko kitendo kilichofanyika ambazo alisema  kimemsikitisha mno

“Nasikitika kama bibi, kama angekuwa hai huyo mtoto wangenipa mimi nimlee kuliko kumtupia kwenye pipa la maji, imeniuma sana,” amesema Aika.

Diwani wa Kata ya Mandewa, Baraka Hamisi amesema hata kama mtoto akibeba ujauzito akiwa mwanafunzi, haifai kuchukua uamuzi huo kwa sababu Serikali imeruhusu binti kurudi shule baada ya kujifungua.

“Ninalilaani sana, mimi nawaasa wananchi hata kama binti wako amepata mimba na ni mwanafunzi, basi wasichukue hatua mbaya kama hii kwa sababu bado anaweza akalea mtoto na akarudi shuleni,” amesema diwani.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.