Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

kubeba mimba baada ya kufungwa kizazi inawezekana?

kubeba mimba baada ya kufungwa kizazi inawezekana?

Madaktari walipomshauri Beth McDermott asizae watoto tena kwa sababu ya matatizo ya uti wa mgongo uliokuwa na uchungu usio kifani, aliamua kufungwa kizazi.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 31 alifanyiwa upasuaji huo wakati mtoto wake wa kiume wa pili, Corey, alipozaliwa kwa njia ya upasuaji msimu wa joto uliopita.

Lakini miezi michache baadaye, aligundua kuwa alikuwa mjamzito tena.

“Nilihisi kuumwa kidogo na nikafikiri labda ni mwili wangu tu uliokuwa unaendelea kuzoea hali kutokana na upasuaji wa kufunga uzazi. Sikufikiria hata kidogo kuwa nilikuwa na ujauzito,” mama huyu anayeishi Edinburgh, Scotland, aliambia BBC.

“Nilipogundua kuwa nina ujauzito, nilipatwa na mshtuko, nikahema kupita kiasi na kushindwa kupumua. Mume wangu alikuwa akipiga simu akiniambia nitulie…”

Vipimo vitano vya ujauzito na uchunguzi wa dharura wa hospitali ulithibitisha kuwa Beth na mumewe Shaun, 31, walikuwa wanatarajia mtoto wao wa tatu.

Hospitali ya taifa ya Scotland iliomba msamaha kwa Beth na familia yake na kusema utaratibu wa kufunga uzazi ulikuwa na ufanisi zaidi ya 99%. Hata hivyo, Beth sasa anataka uchunguzi ufanywe ili kufahamu kilichotokea.

Beth alifungwa kizazi (kwa kutumia klipu za chuma zilizounganishwa kwenye mirija yake ya uzazi) baada ya kulazwa hospitalini mara kadhaa wakati wa ujauzito wake kwa watoto wawili waliotangulia, na kuishia kwenye kiti cha magurudumu.

Mimba hizo zilizidisha hali ya maumivu ya mgongo ambayo Beth aliugua, na kumsababishia kupooza kuanzia kwenye kiuno kwenda chini.

Aligunduliwa mwaka wa 2014 na kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo.

“Sikuweza kutembea kwa miezi sita, kisha ilinibidi nifanyiwe tiba ya mwili kwa muda wa miaka miwili na nusu hadi nikaanza kutembea kwa usaidizi, ambao nyakati fulani bado nahitaji usaidizi huo hadi leo,” anaeleza.

“Kibofu changu pia hakitaweza kujirekebisha. Maisha yangu yalibadilika kabisa kwa siku moja.”

Ingawa Beth ni mlemavu, alijifunza kutembea tena kwa magongo baada ya kukaa kwa miezi sita kwenye kiti cha magurudumu na kisha kutumia kitembezi.

“Bado huwa napata maumivu kila siku,” anasema.

Madaktari walimwambia huenda hataweza kupata watoto, lakini wenzi hao walikuwa wamepata mtoto wao wa kwanza, Sonny, miaka sita iliyopita.

“Nilipopata ujauzito, sikutarajia. Nilifurahi kwa sababu sikuwa na uhakika kama ningeweza kupata watoto,” aliongeza.

Kufunga uzazi kwa wanawake kuna ufanisi zaidi ya 99%

“Tuliogopa kwa sababu madaktari walisema ujauzito haungekuwa rahisi, niliogopa lakini tuliamua kujaribu,” anakumbuka: “Kwa kawaida mimba huwa na maumivu mgongoni. Kwa upande wangu ilikuwa uchungu zaidi na iliniathiri sana kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Nilikuwa hospitali kila wakati na ilinibidi nitumie kiti cha magurudumu tena.”

Wanandoa hao sasa wana mtoto wa miezi saba Corey.

“Ilikuwa vigumu sana kuamua kufunga kizazi lakini nilikuwa na hofu ya kupata ujauzito tena wakati ambapo mimba mbili za awali zilisababisha maumivu makali kutokana na ugonjwa wangu,” anaeleza.

“Kwa hiyo nilikasirika kidogo kwa kuamini kuwa utaratibu huu wa kufunga kizazi ungemaliza hili,” Beth anakumbuka na kuongeza: “Wiki chache za kwanza nilivunjika moyo. Tayari nilikuwa nimefanya uamuzi mgumu wa kufunga kizazi; lakini pia, nililazimika kufanya uamuzi mwingine mgumu, ule wa kutoa mimba yangu.”

Hatimaye, wanandoa hao wakaamua kuwa Beth atajifungua.

“Kufanya uamuzi huu wakati nikiwa nimemshikilia mtoto wangu wa miezi saba huku nikiwa ninamuangalia machoni ilikuwa hatua ngumu sana maishani mwangu.”

Sasa, Beth anataka madaktari kuchunguza nini kilitokea, lakini hospitali inasema, huwa inaarifu wahusika kuwa machakato huo unaweza kufeli kwa asilimia 1 ya wanawanake kati ya wale wanaofanyiwa.

Mkurugenzi wa matibabu wa Hospitali kuu ya Scotland Dk Tracy Gillies alisema: “Tunasisitiza hadharani pole zetu za dhati kwa Bi McDermott na familia yake kwa dhiki iliyosababishwa.”

Aliongeza: “Kufunga uzazi kwa wanawake kuna ufanisi wa zaidi ya 99%; hata hivyo, kuna hatari ndogo kwamba operesheni ya kufunga kizazi haitafanya kazi, kwani mirija iliyoziba inaweza kuziba mara moja au miaka kadhaa baadaye. Hatari hizi hujadiliwa na wagonjwa wote kabla ya utaratibu.”

“Bi McDermott bado anawasiliana na timu zetu na tunamhimiza atoe wasiwasi wowote na sisi.”

Beth alipokea msamaha wa maandishi kutoka hospitali kuu huko Scotland.

Beth anasema: “Sasa kwa kuwa nimeondokana na mshtuko, nina furaha, lakini pia nina hofu kwa sababu najua jinsi mimba yangu ya mwisho ilivyokuwa mbaya.”

“Ni miujiza na kuna sababu kwanini nimepata ujauzito wa mtoto huyu. Natumai ni wa kike, lakini muhimu ni kwamba mtoto wetu ni mzima na buheri wa afya,” alisema na kuongeza: “Ijapokuwa nimepata msamaha wa maandishi, haitoshi. Nataka majibu.

“Nataka kujua ikiwa mchakato huu ulifeli kwa sababu niko kwenye kundi la asilimia 1 au kuna kitu ambacho hakikufanywa kwa njia stahiki wakati wa upasuaji. Ningependa uchunguzi ufanywe na hili ndio lile ambalo nitaomba hospitali kuu lifanyike siku za usoni.”

Via:Bbc

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.