Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kutokwa na maji ukeni yasiyo na harufu

Kutokwa na maji ukeni yasiyo na harufu

Kutokwa na Maji ukeni yasiyo na harufu sio tatizo  hii huweza kuwa njia mojawapo ya asili ambapo Uke hujisafisha wenyewe. Mara nyingi maji haya yanakuwa na rangi nyeupe na hayana harufu yoyote.

Tabia hizi za haya maji huweza kubadilika kulingana na vipindi, mfano kwenye vipindi ya hedhi,mimba n.k.

Kumbuka; Ikiwa maji haya yakabadilika ghafla na kuwa na harufu au rangi isiyoeleweka, wingi wake kuongezeka n.k hakikisha unapata msaada wa vipimo na tiba maana hizi ni dalili za maambukizi ya magonjwa na siokawaida.

Haya ni baadhi ya maambukizi ambapo mara nyingi huweza kuhusishwa na hali hii(Potential infections);

  • Maambukizi ya bacteria Ukeni,(bacterial vaginosis)
  • Fangasi sehemu za Siri(candidiasis)
  • Tatizo la trichomoniasis
  • Ugonjwa wa chlamydia
  • Ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea)
  • genital herpes n.k

Ikiwa mtu anahisi ana hali yoyote kati ya hizi hapa, anashauriwa kuonana na wataalam wa afya kwa ajili ya matibabu,

Pia Mwanamke anaweza kutokwa na maji maji Zaidi ukeni ikiwa ana hali kama hizi;

– Mjamzito

– Anatumia vidonge vya uzazi wa mpango

– Ana hisia kali za kufanya mapenzi(sexually active) n.k

Kipindi cha Ujauzito:

Ni muhimu sana kuwa macho na kutokwa na maji au uchafu ukeni wakati wa ujauzito. Jihadhari na mabadiliko yoyote, ikiwa ni pamoja na:

– tofauti katika harufu, rangi, au texture

– maumivu yanayoambatana na kutokwa na maji maji au uchafu ukeni

– maumivu au kuwasha kwenye eneo la uke

Hizi zinaweza kuashiria hali zinazohitaji matibabu. Wasiliana na wataalam wa afya.

Kabla ya period:

Mabadiliko huweza kutokea pia kipindi cha hedhi,

Wakati Yai linajiandaa kutoka na wakati linatoka mwanamke huweza kutokwa na ute ute ambao huvutika.

Baada ya period

Mara tu baada ya kumaliza hedhi, Mwanamke huweza kutoa uchafu wenye rangi kama brown kutokana na mabaki ya damu Ukeni.

Matibabu ya Tatizo hili

Ikiwa maji maji yanatoka Ukeni lakini yanaambatana na dalili zingine kama vile;

Kuumwa sana tumbo, kutoa harufu ukeni, kupata muwasho,maji kubadilika rangi n.k, hakikisha unapata matibabu.

Na matibabu yake yatategemea chanzo chake husika, Mfano;

✓ Kama tatizo ni maambukizi ya bacteria Ukeni(Bacterial vaginosis): mgonjwa huweza kupewa dawa jamii ya antibiotic kama vile; clindamycin cream/oral au intravaginal metronidazole.n.k

✓ Kama ni Trichomoniasis: Mgonjwa atapewa pia Oral Antibiotics

✓ Kama ni Fangasi(Candidiasis): Mgonjwa atapewa dawa za kutibu Fangasi n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.