Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Manusura wa ajali ya ndege waliokula maiti za wenzao ili waishi

Manusura wa ajali ya ndege waliokula maiti za wenzao ili waishi

Timu ya raga ya shule ya Old Christians Club kutoka Montevideo, Uruguay ilikodi ndege ya Jeshi la anga la Uruguay kusafiri Oktoba 13, 1972 hadi Santiago, Chile.

Wakisafiri kwenda kucheza mechi dhidi ya Old Boys katika jiji hilo. Ndege yao FH-227D, iliyokuwa na abiria 45, ilipokuwa ikivuka Milima ya Andes, ilianguka na kusababisha vifo vya papo hapo vya watu 12.

Wengine 17 walikufa siku zilizofuata, kutokana na majeraha, ukosefu wa chakula na hali mbaya waliyokabiliana nayo.

Ajali hiyo ilipachikwa jina la “Muujiza wa Andes” na imeonyeshwa katika filamu ya Netflix “The Snow Society.”

Hili Ni moja ya tukio la kushangaza katika historia ya anga kwani watu16 walionusurika ni kwa sababu walikula miili ya wenzao waliokufa. Waliokolewa siku 72 baada ya ajali hiyo.

Mmoja wa waliookolewa, Roberto Canessa, sasa ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto. Alihojiwa na BBC, Machi 2016, baada ya kutoa kitabu chake cha ushuhuda wa tukio hilo.

Tukiwa katika anga ya Andes kulikuwa na mawingu sana. Wakati fulani mmoja wa wahudumu wa ndege aliwaambia abiria “fungeni mikanda, tutapitia katika mawingu na ndege itatetemeka.”

Hakika, ndege ilianza kutetemeka. Kuna mtu aliniambia nichungulie dirishani, ndege ilikuwa ikipaa karibu sana milima.

Ndege ilijaribu kupaa kwenda juu urefu, lakini ilianguka. Nilishikilia kiti changu bara’bara. Ndege ilipoteza mabawa yote mawili na kuanza kuteleza chini ya milima.

Hatimaye iliposimama, niliruka kwa nguvu na niligonga kichwa changu kwenye ardhi kwa nguvu na kuhisi kama nitazimia. Sikuamini kwamba ndege ilikuwa imesimama.

Niliona miguu yangu bado ipo, mikono yangu bado ipo, nimeokoka.

Sikuweza kuamini. Niliangalia pande zote na kila kitu kimetawanyika. Baadhi ya marafiki walikuwa wamekufa, wengine walijeruhiwa, wakivuja damu, wengine walikuwa na vipande vya vyuma miilini mwao.

Nilijisemea ni lazima niondoke hapa, polisi watakuja, magari ya kubebea wagonjwa yatakuja, askari wa zima moto, nikaenda kwenye mkia wa ndege.

Ndege ilivunjika na nilipokwenda kwenye theluji, nilihuzunika sana kwa sababu tulikuwa katikati ya milima, tukiwa tumezingirwa na ukimya mkubwa.

Hakukuwa na msaada wowote

Canessa na manusura wengine 15 walilazimika kutembea kwa siku 11 ili kuokolewa.

Rubani alikuwa hai, lakini alinasa kwenye chumba cha marubani. Hawakuweza kumtoa na akasema “Kuna bunduki kwenye mkoba wangu.” Alitaka kujiua. Aliugulia uchungu usiku kucha. Hatukuweza kumtoa.

Baridi ilikuwa kali. Siku iliyofuata, kwa vile alijeruhiwa vibaya alifariki. Nilijisikia vyema kwa sababu alikuwa akipata mateso na maumivu makali.

Kwa wale waliobaki, kulikuwa na miamba na theluji tu. Hakukuwa na chakula na tulihisi njaa. Kuna hisia ndani yako inakwambia unapaswa kula kitu. Kwa hiyo tulifikiria kula ngozi ya viatu au kamba.

Tulianza kutafuna ngozi, lakini tulihisi ilikuwa na sumu, kwa sababu ilikuwa na kemikali nyingi. Kwa hiyo hatukuweza kuendelea kutafuna.

Mtu mmoja wakati fulani alisema, “Nadhani nimepata wazimu, kwa sababu nafikiria kula miili ya marafiki zetu.”

Walijibu huo ni wazimu, hatutafanya hivyo, hatutakula nyama za watu.

Wakati huo, nilikuwa mwanafunzi wa udaktari na niliona nyama, mafuta, protini, wanga. Ilikuwa vigumu kwangu kukata sehemu ya miili yao.

Mtu mwingine alisema , “ikiwa Yesu Kristo alisema kwenye Karamu ya Mwisho uchukue mwili wangu na damu yangu.”

Lakini kwangu haikuwa Karamu ya Mwisho. Ingawa wakati huo nilijiuliza ninge “waza” nini ikiwa ningekuwa mmoja wa maiti.

Ningejivunia kwamba mwili wangu ulitumiwa na marafiki zangu kwa riziki. Leo nahisi nina sehemu ya marafiki zangu ndani yangu na sina budi kushukuru kwa kumbukumbu zao.

Kula miili ili kuishi muda mrefu zaidi ili kuokolewa, ilikuwa vigumu kwa wengine lakini rahisi kwa wengine.

Mara ya kwanza ilikwua kama majaribio. Kisha ikawa kawaida kukata nyama na kugawana kati ya waliosalia.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.