Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mwimbaji/Mwigizaji Marianne Namshali Mdee ( Mimi Mars ) tayari ameruhusiwa kutoka Hospitali

Mwimbaji/Mwigizaji Marianne Namshali Mdee ( Mimi Mars ) tayari ameruhusiwa kutoka Hospitali na sasa yuko nyumbani akiendelea vizuri kiafya baada ya kupata ajali ya gari zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Mars ambaye alipata ajali hiyo siku chache baada ya kuachia ngoma yake ya tatu kwa mwaka 2023 ‘samaleko’, ameendelea kuimarika kiafya kwa kiwango kikubwa hadi kuweza kuongea japo hadi sasa Madaktari wamemzuia kushika simu yake.

Dada yake ( @vanessamdee ), amepost video na picha zinazomuonesha akiwa amekuja Dar es salaam kwa muda mfupi na kuondoka kurudi Marekani anakoishi baada ya hali ya Mimi Mars kuonekana kuwa imara.

Ndani ya video hiyo kuna sehemu ikiwaonesha wakiwa pamoja Hospitalini huku wakicheza karata na kufurahi pamoja na Mimi Mars aliyekuwa amejilaza katika kitanda…… wakati huu afya ya Staa huyo ikiendelea kuimarika imeelezwa kuwa atakuwa akitembelewa na Daktari nyumbani mara mojamoja kwa ajili ya kujua maendeleo yake.

Much love kwako Favorite @mimi_mvrs11 ! tunazidi kukuombea afya kamili na kurejea kwenye mitikasi yako kama kawa Chugga Queen.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.