Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Wananchi Kuondoka maeneo hatarishi

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi waishio kwenye maeneo hatarishi kuondoka katika maeneo hayo ili kuliepusha taifa na maafa yatakonayo na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Akizungumza katika ibada maalum ya kumuingiza kazini Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Malasusa Jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema mamlaka ya hali ya hewa ilishatoa taarifa juu mvua zinazonyesha hivi sasa na serikali imechukua hatua mbalimbali kwenye maeneo yaliyoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua hizo.

“Serikali tayari imeelekeza wizara zote likiwemo jeshi la uokozi kuwa tayari muda wote ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mvua,” amesema Rais Samia

Aidha ametoa pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu na mali zao kutokana na mafuriko yaliyojitokeza kwenye maeneo yao.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.