Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Events

Upasuaji kwa njia ya tundu dogo wa kurekebisha mishipa ya damu iliyotanuka wafanyika

Upasuaji kwa njia ya tundu dogo wa kurekebisha mishipa ya damu iliyotanuka wafanyika

Kwa mara ya kwanza wataamu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanya upasuaji kwa njia ya tundu dogo wa kurekebisha mishipa ya damu iliyotanuka na kupasuka sehemu ya kifua na tumbo kwa wagonjwa watano wenye matatizo hayo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema wagonjwa wenye matatizo hayo wengi wao walikuwa wakipoteza maisha na wale ambao walikuwa wanapona walipewa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Dk Kisenge alisema upasuaji huo umefanywa na madaktari wazawa kwa kushirikiana na madaktari kutoka India na tayari mgonjwa mmoja  alishafanyiwa upasuaji huku wengine watatu  watafanyiwa upasuaji huo leo na mmoja kesho.

“Kwa mara ya tatu tunavunja rekodi tumefanya matibabu makubwa ya kurekebisha mishipa ya damu ambayo imetanuka na kupasuka hii ni tatizo ambalo watu wengi wanalipata na kupoteza maisha ghafla  na wanaobaki tunawapeleka nje ya nchi lakini hivi  sasa tutaanza kuwahudumia hapa nchini”,.

“Ni upasuaji mkubwa kufanyika Tanzania na Afrika Mashariki na Kati tumevunja rekodi tunampongeza Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapenda wananchi wake na kutoa  kiasi cha shilingi milioni 900 za matibabu ya kibingwa katika Taasisi yetu,”, alisema Dkt. Kisenge.

Mkurugenzi huyo Mtendaji ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema  mishipa ya damu ya tumboni na kifuani kutanuka na kupasuka kunasabahishwa na vitu vingi ikiwemo shinikizo la juu la damu  ambayo haitibiwi vizuri,uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe uliokithiri na uzito mkubwa.

Dkt. Kisenge alisema katika Taasisi hiyo kuna wagonjwa wapatao 30 wanaosubiri kupata matibabu hayo ambapo gharama zake ni shilingi milioni 80 endapo mgonjwa atatibiwa hapa nchini na milioni 150 akitibiwa nje ya  nchi.
“Tutaendelea kutoa matibabu haya na tutaendelea kuwa na matibabu mapya mengine kwani wataalamu wetu wanajifunza kila siku. Upasuaji huu tulioufanya ukifanyika kwa njia ya kufungua kifua unachukua saa nane ila kwa njia ya tundu dogo ni saa mbili hii ni njia nzuri japo gharama ni kubwa ila Mhe. Rais wetu ametoa  fedha ili wananchi wasaidiwe”, alisema Dkt.Kisenge.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.