Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa wa zinaa pangusa,chanzo,dalili na Tiba

Ugonjwa wa zinaa pangusa,chanzo,dalili na Tiba

Pangusa ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa ambayo hutokea kwa jinsia zote mbili(mwanaume na mwanamke),

Ugonjwa huu husababishwa na bacteria wanaojulikana kama Haemophilus ducreyi(H.ducreyi).Na hutibiwa kwa dawa jamii ya antibiotics.

Dalili za Pangusa

Kwenye hatua za mwanzo,Maambukizi haya huweza kusababisha dalili chache, na unaweza hata kuzipuuzia maana sio kali, ndyo mana kuna umuhimu wa kufanya Screening mara kwa mara.

UGONJWA WA PANGUSA(,chanzo,dalili tiba)

Ugonjwa wa pangusa ni ugonjwa wa zinaa au ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya kufanya ngono, na ugonjwa huu kwa kitaam hujulikana kama chancroid.

CHANZO CHA UGONJWA WA PANGUSA

Ugonjwa wa pangusa husababishwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa ikiwa ni pamoja na Backteria jamii ya Haemophilus ducreyi.

Bacteria hawa husambazwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana.

DALILI ZA UGONJWA WA PANGUSA NI PAMOJA NA;

– Mgonjwa huanza kuwa na viupele sehemu za siri ambavyo baadae huchubuka na kuwa vidonda

– Mgonjwa kupata maumivu makali kwenye vidonda hivi

– Mgonjwa kuhisi muwasho kwenye vidonda

– Vidonda hivi hutoa damu pale vinapoguswa au kubinywa

– Joto la mwili la mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

– Mgonjwa kukosa hamu ya kula chakula

– Na wakati mwingine mgonjwa kupata shida wakati wa kutembea

– kupata maumivu wakati wa kukojoa

– Kutokwa na uchafu(discharge) kwenye uume au Ukeni

– Kupata maumivu wakati wa tendo kwa wanawake

– Kutoa damu(blid) katikati ya period na baada ya tendo la ndoa

– Kupata maumivu kwenye korodani

– Kupata maumivu sehemu ya haja kubwa n.k

MAMBO YA KUEPUKA ILI KUJIKINGA NA UGONJWA HUU WA PANGUSA

– Epuka kufanya ngono zembe(mapenzi bila kinga au condom)

– Epuka tabia ya kuwa na wapenzi wengi

– Epuka tabia ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile

– Kamuone mtaalam wa afya baada ya kuhisi haupo sawa

MATIBABU YA UGONJWA WA PANGUSA

✓ Matibabu sahihi ya ugonjwa wa pangusa huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali kama vile Azithromycin na Doxcycline kutwa mara mbili kwa siku 7 au siku 14.

✓ Matibabu mengine ni pamoja na Dawa jamii;

  • Azithromycin,
  • Ceftriaxone
  • Ciprofloxacin,
  • Erythromycin,

“KUMBUKA; Hakikisha unapata maelekezo kutokwa kwa Mtaalam wa afya kabla ya matumizi ya dawa yoyote,ili kuona ni tiba gani sahihi kulingana na hali yako

Je,chancroid inaweza kupona yenyewe?

Ikiwa una Pangusa au chancroid na hujatibiwa ukapona, vidonda au sores vinaweza kuisha vyenyewe ndani ya mwezi mmoja au miwili, Ingawa utakuwa kwenye hatari ya kupata tatizo lingine la suppurative lymphadenitis, Maambukizi kwenye Soft Tissues.”

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass