Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Elimu&Ushauri

Vyakula vinavyoongeza hamu ya tendo na uboreshaji sawa na dawa ya Viagra

Vyakula vinavyoongeza hamu ya tendo na uboreshaji sawa na dawa ya Viagra

Chokoleti, stroberi, chaza; huelezwa ni vyakula vinavyoweza kuongeza hamu ya kufanya mapenzi na kuboresha ufanyaji wa tendo lenyewe. Lakini kuna ukweli wowote kwenye madai hayo?

Kwa wale ambao wana matatizo na ufanyaji wa mapenzi, ni kweli vyakula fulani vinaweza kusaidia kwa njia sawa na dawa ya Viagra.

Jamii mbalimbali katika historia zimetafuta vyakula ambavyo vinaweza kuongeza hamu ya kufanya mapenzi au kuboresha utendaji wa ngono.

“Hata hivyo, watu walio na matatizo katika kufanya mapenzi ndio huona mabadiliko wanapokula hivi vyakula,” anasema Lauri Wright, msemaji wa Chuo cha Nutrition and Dietetics, kutoka Marekani. “Mtu asiye na matatizo hawezi kuona mabadiliko yoyote.”

Chakula kimoja ambacho kinaaminika kwa muda mrefu kuongeza hamu ya ngono ni chokoleti. Utafiti unaonyesha kuwa kakao pia inaweza kuongeza hamu.

#Soma pia vyakula vinavyopunguza nguvu za kiume

Kula chokoleti kunaweza kuongeza hamu ya tendo kwa kuchochea utengenezaji wa serotonini na kemikali ya dopamini kwenye nyurotransmita, ambazo pia huchangia katika kuwa na hisia za kimapenzi.

Mtindo wa maisha na lishe

Michael Krychman, mtaalamu na mshauri wa masuala ya kujamiiana kutoka kliniki ya Sexual Health and Survivorship Medicine, Marekani anasema “tunachojua ni kwamba, watu wanaofanya mazoezi, kula lishe bora na kupunguza msongo wa mawazo, vitu hivi vyote huboresha uwezo wa kufanya tendo.”

“Mlo wetu unaweza kufanya kazi kama kichochezi kutupa manufaa kama vile mtiririko mzuri wa damu, kuongezeka homoni au kuongeza hamu,” anasema Wright.

“Jambo la msingi kuzingatia ni vyakula kama samaki, nyama isiyo na mafuta, karanga, matunda, mboga mboga na nafaka, ambavyo husaidia kazi ya neva na kusaidia mtiririko wa damu na homoni,” anasema Wright.

“Hamu ni ya kimwili na ya kisaikolojia. Ukweli kwamba hamu ya kufanya ngono ina mambo mengi. Dawa au chakula vinaweza kufanya kazi,” anasema Nan Wise , mtaalamu wa saikolojia na masuala ya kujamiina katika Chuo Kikuu cha Rutgers huko New Jersey.

“Uzoefu wetu pia unaweza kuchangia kujua ni vyakula gani vinavyoongeza hamu ya kufanya tendo kwa mtu mmoja mmoja,” anasema Jean-Christophe Billeter, profesa wa tabia za kijamii na kujamiiana katika Chuo Kikuu cha Groningen nchini Uholanzi.

“Ubongo unakuwa na waya wa kutengeneza kumbukumbu tunapopata mafanikio ya tendo la ndoa, kulingana na hali itakavyotokea katika mazingira ambayo mtu alifanya ngono, hii itakua ni kitu cha kuamsha hamu ya kufanya mapenzi katika siku za usoni.”

Kuna utafiti unapendekeza kuwa mawazo chanya yanahusishwa na kuongezeka kwa msisimko wa ngono, na lishe iliyo na vyakula vingi vya mimea.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass