Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

“Alimuomba mama yangu mkasi, akakata nywele zangu na kumwambia: ‘Mfanye kama mvulana

Uso wa Nilofar Ayoubi, mwenye umri wa miaka 4 tu, bado ulikuwa mwekundu kutokana na kofi alilokuwa amepigwa na mgeni wakati akicheza katika mitaa ya Kunduz, kaskazini mwa Afghanistan. Pigo hilo lilikuwa la kikatili sana kiasi kwamba alianguka sakafuni.

“Nilirudi nyumbani nikilia baba yangu alikuwa mwekundu kwa hasira,” Nilofar ameiambia BBC, miaka ishirini na mitatu baada ya tukio hilo ambalo anasema limewekwa katika kumbukumbu zake. “Namkumbuka akirudi nyuma na kukasirika, akipiga kelele na kusema ‘anawezaje kukugusa?'”

Muda mfupi kabla ya kumpiga, mgeni huyo alikuwa amemgusa kifua chake, akitafuta ishara za “uke.” Kisha akamtishia na kumwambia kwamba ikiwa hatavaa kilemba chake, wakati mwingine, angemshambulia baba yake.

Baada ya muda mfupi wa hasira, baba yake Nilofar alifanya uamuzi mkali: “Alimuomba mama yangu mkasi, akakata nywele zangu na kumwambia: ‘Mfanye kama mvulana.'”

Nilofar alikulia Afghanistan wakati wa enzi ya kwanza ya utawala wa Taliban – kuanzia mwaka 1996 hadi 2001 – na kwa karibu miaka 10, aliishi maisha ya mtoto, akitoroka udhibiti wa ukandamizaji ambao Sharia, sheria za Kiislamu, zinazokandamiza wanawake.

Leo, akiwa uhamishoni, anakumbuka jinsi mambo yalivyokuwa wakat iwa makuzi yake katika moja ya maeneo ya kihafidhina zaidi duniani, ambayo jinsia unayozaliwa nayo inafafanua mipaka ya haki unazoweza kupata.

Tofauti kati ya maisha ya mvulana na msichana nchini Afghanistan mara nyingi ni mbaya.

Kukulia katika Kunduz

Nilofar alizaliwa mwaka 1996, lakini nyaraka zake za utambulisho zinasema alizaliwa mwaka 1993. Baba yake alifanya mabadiliko hayo ili binti yake aweze kuanza shule haraka iwezekanavyo baada ya Marekani kuingilia kati mwaka 2001 kuipindua serikali ya Taliban.

” Kunduz sio mji wa kuvutia kwa mwanamke kukulia katika .”Ni vigumu kuwa mwanamume, na ni vigumu zaidi kuwa mwanamke,” aliiambia BBC.

“Kama mtoto, una nguvu moja kwa moja, hata kama wewe ni mtoto wa miaka 2 inamaanisha unapokea heshima zaidi kuliko mama yule yule aliyekuzaa. Kuanzia umri wa miaka 4, unaweza kuwa msimamizi wa kisheria wa mwanamke ambaye kuletwa wewe katika dunia (…) na yeye ni mtumwa wako. “Kama wewe ni mwanamke, wewe ni asiyeonekana.”

Chini ya sheria kali kama hizo kali , Nilofar anaeleza kuwa ilikuwa kawaida kwa familia yao kuwavalisha mabinti zao kama wavulana hasa kama familia haikuwa na mtoaji wa msingi: chini ya sharia, mwanamume yeyote anaweza kumkaribia mwanamke ambaye hana wa kumhudumia na kumlazimisha kuwa mke wake wa tano au wa sita.

“Kwa upande wangu, hali ilikuwa tofauti. Haikuwa kwa kukosa mtoa mtu wa kunisaidia lakini ilikuwa ni kuweza kuishi maisha kwa uhuru.”

Nilofar anakumbuka msaidizi wao , baba yake, alikuwa mtu maalum kwa wakati huo nchini Afghanistan: “Alichukia siasa.”

Utawala wa Taliban unaweka sheria kali ya Sharia, inayozuia haki nyingi za wanawake.

Akiwa amesimama mbele ya baba yake, huku nywele zake zikiwa zimenyolewa na kuvaa nguo za mmoja wa ndugu zake, Nilofar alikuwa karibu kuanza maisha tofauti kabisa na ya wasichana wengine wa umri wake, wakiwemo dada zake.

“Nilianza kuishi maisha kama ya kaka zangu, niliweza kwenda na baba yangu sokoni nikiwa nimevaa kama kijana. Tuliweza kutembea kwa maili na maili. Tulienda kwa basi kutazama michezo, nilikuwa na marafiki katika kitongoji na nilitumia muda wote kucheza mitaani.”

Dada zake, kwa upande mwingine, walilazimika kufunika nywele zao – hata ndani ya nyumba – na kuvaa kihafidhina, kitu ambacho baba yao alichukia.

“Baba yangu hakuwahi kukubaliana na suala la sisi kuvaa nguo hizo nyumbani, siku zote alipigana na mama yangu na kumuuliza kwa nini hakuvaa vizuri. ” Nguo hii ni ndefu sana, kwa nini ni pana sana? “Baba yangu alikuwa mtu wa aina yake .”

Kwa miaka mingi, baba yake Nilofar alipokea vitisho.

Kujenga uaminifu

Kukua katika ulimwengu wenye vitambulisho viwili, Nilofar daima alihisi utofauti. Labda yule ambaye angeweza kuelewa vizuri kile alichokuwa akipitia alikuwa jirani yake, msichana wa umri huo ambaye pia alivaa kama mvulana na ambaye alifanya maovu mengi.

“Tulikuwa tunafanya mambo sawa. Wakati wowote walipokuwa wakikaribia kumkamata mmoja, mwingine alikuja kumuokoa,” anasema Nilofar, akisisitiza kuwa hatari ya kutambuliwa kama wanawake ilikuwa ya mara kwa mara.

“Pia ilinisaidia sana kwamba nilikuwa na uhakika kuwa nilikuwa mvulana kwamba ilikuwa vigumu kwa watu kufikiri sikuwa nilivyo. Nakumbuka kwamba katika mikutano, mimi ndiye niliyesema”‘acha tuwasumbue wasichana’, nikiwaambia, ‘oh wewe ni mrembo, jinsi ulivyo mzuri tena mzuri sana.'”

Maisha ya Nilofar yalikuwa ya kucheza karate, judo na kuendesha baiskeli, wakati dada zake wakiishi na kucheza michezo ya kawaida ya wasichana Kunduz, kukaa nyumbani, kuishi maisha ya kimya kimya na nje ya macho ya wanaume.

“Sikuwahi kuwa na uhusiano na dada zangu. Sikuwahi kuelewa jinsi dunia yao ilivyokuwa. Na ndio maana sikujua kwamba wasichana walipata hedhi.”

Nilofar alikuwa ameona matangazo ya kuuza taulo za hedhi, lakini haikuwa wazi kwake kazi yake ilikuwa nini.

“Mara tu nilipopata taulo za hedhi nikaenda kwa baba yangu: ‘Baba, baba, angalia, ni kama wale kwenye TV, ni ya kuchekesha. Ni kwa ajili ya nini?’ “Baba yangu hakujua la kunijibu.”

“Baada ya hapo nilimpelekea kwa dada yangu. Nakumbuka alichukua kutoka kwangu na alinitukana. Hata wakati huo, hakuna mtu aliyefikiria kuniambia hedhi ni nini.”

Nilofar anasema uzoefu wake kama mtoto ulimpa ujasiri kwamba kamwe asingekua kama msichana.

Kurejea katika ukweli halisi wa jinsia yake

Akiwa na umri wa miaka 13, na baada ya kucheza judo kwenye jua kali la mchana, Nilofar alirudi nyumbani akiwa amechafuka: miguu yake iliumia na alitaka kulala chini. Alipoingia bafuni na kuona kwamba alikuwa anavuja damu, alikuwa na wasiwasi, lakini hakufikiria kwamba kile kinachokuja kitabadilisha maisha yake.

“Siku iliyofuata nilimwambia rafiki yangu. Alicheka na akaniuliza iwapo nilikuwa mjinga, kama dada zangu hawakuwa wameniambia chochote.”

“Nilipofika nyumbani, mama yangu aliona kitu kwenye nguo zangu na badala ya kunikumbatia na kunifariji, alikuwa akinilaani na kuniuliza ‘Kwa nini umekua haraka sana?'”

Mama yake Nilofar alianza kulia kwa sababu alijua kwamba siku za usoni alimsubiri binti yake kama yeye na binti zake wengine, waliofungwa ndani ya kuta nne za nyumba yake.

“Alikuwa amezoea wazo kwamba angeweza kuhisi kuwa nina uhakika kwamba niko salama na huu ndio wakati alipogundua kuwa yote yalikuwa bure.”

Nilofar alianza mchakato mwingine wa kiwewe, wakati huu, akichukua halisi ya utambulisho wa jinsia ambayo alikuwa amezaliwa: “Tulikuwa na hadithi hii kwamba ikiwa ungeenda chini ya upinde wa mvua, jinsia yako ingebadilika.”

Kufuatia kuanguka kwa Taliban mwaka 2001, wasichana waliweza kurudi madarasani nchini Afghanistan.

Miaka ya kuishi kama mwanamume iliashiria utambulisho wa jina Nilofar, na kumpa usalama ambao wasichana wengine shuleni mwake hawakuwa nao.

Afghanistan ilikuwa ikipitia kipindi kipya cha ukosefu wa utulivu wa kisiasa, kufuatia uingiliaji wa Marekani nchini humo baada ya Septemba 11, 2001.

Serikali mpya ilikuwa imewekwa na ilikuwa ikijitahidi kudumisha udhibiti, lakini baadhi ya haki, kama vile elimu, zilianza kuwafikia wanawake.

Nilofar aliweza kwenda shule, ingawa alibaki na roho hiyo ya uasi tangu utotoni wake.

“Niliunda kikundi hiki kinachoitwa ‘Niñas del Norte’. Na kupitia kundi hilo, tulianza harakati zetu za kuwaelimisha wasichana shuleni kuhusu mambo ambayo hawakufundishwa, kama kubalehe.”

“Kila kitu ni mwiko kwa msichana nchini Afghanistan, ikiwa ni pamoja na hatua zinazosababisha kuwa mwanamke wakati mwili unapoanza kubadilika. Wasichana wana aibu sana kuhusu mabadiliko haya ya ukuaji wao.”

Licha ya ziara zake mbalimbali katika ofisi ya mkurugenzi, utendaji wa kitaaluma wa Nilofar ulikuwa wa kushangaza na hilo lilifungua milango kwa yake ya kuweza kusoma nje ya nchi, nchini India.

Ilikuwa wakati huu katika maisha yake, wakati alipokuwa akifanya kazi bila kuchoka kuelekea shahada ya uzamili, ndipo alipoanza alifikiria wazo la ndoa.

“Kwa kuwa nilikuwa mdogo nilipokea maombi mengi, ambayo baba yangu aliyajibu kila wakati ‘Usithubutu kumkaribia.’ Yeye si wa kuolewa kwa sasa, atamaliza masomo yake na kisha achague yeye mwenyewe bwana wa kuishi naye’’

Hilo ndilo lililokwama kwenye ubongo wangu, ‘Nitapata shahada ya uzamili na kisha, nitampata mume .'”

Nilofar alifunga ndoa mwaka 2016, alipofikisha umri wa miaka 19, labda, anasema, alikuwa akitaka kujaza pengo lililoachwa moyoni mwake na kifo cha baba yake, ambaye alikufa mnamo 2015.

“Wakati mume wangu aliposema alikuwa sawa na baba yangu wakati huo sikuiona, hakuna mtu angeweza kuwa kama baba yangu, lakini aliishia kuwa karibu kama yeye. Kwa kweli, hakuna mtu anayeweza kuchukua nafasi ya baba yangu, lakini alijaza utupu huo na amenipa msaada mkubwa kama baba yangu alivyonipa. ”

Aliporudi Afghanstan kwa msaada wa mumewe, Nilofar aliuwa mjasiriamali, akibundi mitindo ya mavazi , kuuza samani na alimiliki kampuni ya kuuza mapambo ya ndani ambayo ililenga kutoa kazi kwa wanawake ambao hawakuwa na msaada wa kifedha. Alikuwa na wafanyakazi 300 na maduka kadhaa katika jiji.

Kutoroka

Kurejea kwa Taliban madarakani nchini Afghanistan mnamo Agosti 2021 kulizua hofu na sintofahamu miongoni mwa watu wanaotaka kuondoka nchini humo.

Licha ya mafanikio ya kifedha ambayo familia ya Nilofar ilikuwa nayo nchini Afghanistan, hali ya kisiasa nchini humo ilianza kuonekana kuzorota kutokana na ukosefu wa usalama.

Na kisha, Agosti 2021 ilifika. Taliban walikuwa wakipata ardhi kwa miezi kadhaa, na mwezi Agosti, walifika Kabul, mji mkuu, tena.

“Mume wangu alipokea simu kutoka kwa waziri wa serikali ambaye alimwambia aandae kitambulisho na pasipoti haraka kwa ajili ya binti yangu,” anasema Nilofar. Mtoto wangu alikuwa na umri wa miezi 11 tu.

Simu pia zilianza kutoka dukani kwake, na wafanyakazi waliokata tamaa hawajui cha kufanya. Nilofar alimpigia simu mtoto wake na kumuomba afunge mizigo yake.

Aliporudi, aliwachukua watoto wake na mizigo yoyote aliyoweza na kuelekea nyumbani kwa mama yake. Lakini vurugu zilitawala katika mji huo.

“Wakati huu niliona mambo ambayo yatanisumbua maisha yangu yote: Nilimuona mtu aliyevalia sare ya polisi kwenye baiskeli akimwambia mwingine: ‘Chukua bunduki yangu, chukua baiskeli yangu, nipe nguo za kiraia.’ Alilia na kusema kwamba walikuwa wamesalitiwa.”

Kwa maelfu ya watu ambao walikuwa wameifanyia kazi serikali inayoungwa mkono na Marekani, kurejea kwa madarakani kwa Taliban -utawala ambao uliadhibu hata makosa madogo zaidi kwa njia za kikatili, kulimaanisha hukumu ya kifo.

Nilofar hakuweza kufika nyumbani kwa mama yake, na alilazimika kujificha na watoto wake katika eneo la karibu, kutoka mahali ambapo – kutokana na roho yake ya uasi – alihojiwa na waandishi wa habari kutoka duniani kote, ambapo aliwaelezea juu ya kile kilichokuwa kikimzunguka.

“Katika mahojiano na mwandishi wa habari kutoka Poland, aliniuliza ikiwa nilikuwa kwenye orodha yoyote ya kuhamishwa kutoka Afghanstan kwenda nchi ya kigeni nikamwambia hapana. Aliniomba kwa muda na alipopiga simu tena, aliniambia kwamba kulikuwa na ndege ya Poland ambayo, labda, inaweza kututoa nje ya nchi.

Maisha mapya

Nilofar na familia yake waliondoka Kabul na wanaamini hawataweza kurudi tena

Nilofar anasema kuwa mwandishi huyo alimwongeza kwenye kundi la WhatsApp na kumwambia kuwa wakati anapopokea simu hiyo, atakuwa na saa 24 za kwenda uwanja wa ndege akiwa na mifuko miwili tu.

“Mama yangu alikuwa huko, na kitabu kitakatifu mkononi mwake. Kuangalia uso wa mama yangu kulionyesha kwamba alijua kuwa hataniona tena. Na hiyo ilikuwa mara ya mwisho kumuona mama yangu, na nyumbani kwetu…”

PICHA: Leo Nilofar ni mwandishi wa habari na anazungumzia hali ya wanawake katika nchi yake ya asili ya Afghanistan.

Na anasema uzoefu wake, baada ya kuweza kuishi maisha ya mwanamume na mwanamke nchini Afghanistan, umekuwa “baraka na laana” kwa kila kitu ambacho kimetokea tangu wakati huo.

“Siwezi kuwa mwanamke wa 100%, wala 100% mwanaume. Lakini ilikuwa baraka kwa sababu niliweza kupata uzoefu wa pande zote mbili na hilo limenifanya kuwa mwanamke mwenye nguvu leo.”

Nguvu ambayo anahitaji kusonga mbele na ndoto yake kuu: “Sitaki kuwa mtu ambaye alizaliwa, aliishi miaka michache na kufa bila kuchangia chochote,” anasema, kufuatia ushauri wa baba yake, mtu huyo ambaye bado yuko naye moyoni mwake leo na hiyo inaelezea maisha yake milele.

“Naweza kuona uso wake. Siku zote aliniambia niache siasa, na kwenda kila mahali kutafuta kuleta mema.”

Baada ya safari ya “kutisha” ya siku tatu, familia iliwasili Poland kuanza maisha mapya. Ilikuwa ni nchi ambayo walikuwa wameisikia taarifa chache kuihusu.

“Ni vigumu sana kutokuwa na familia yoyote hapa. Hasa kwa mwanangu. Anakumbuka Kabul kwa kiasi kikubwa. Ananiuliza kuhusu bibi yake na kuuliza kwa nini hawezi kuwa hapa na sisi.”

Bila majibu ya kuridhisha, kitu pekee ambacho Nilofar anaweza kufanya ni kufanya kazi kwa ajili ya watu walioachwa nyuma, kwa mama yake, wafanyakazi wake na dada ambao hawakuweza kuondoka na ambao leo wanaishi tena chini ya Taliban.

Ametembelea Brussels, Ujerumani na Marekani, akizungumza katika mikutano ya haki za binadamu kuhusu haki za wanawake nchini mwake, na anaendelea kusaidia mashirika ambayo yanawasaidia wanawake wasiojiweza.

Source:Bbc

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.