Bila Maji hakuna Maisha, ni muhimu sana kupata Maji safi na Salama
Bila Maji hakuna Maisha, ni muhimu sana kupata Maji safi na Salama,
Uchafuzi wa Mazingira pamoja na kukosa Maji Safi ni chanzo kikubwa cha watu kuendelea kupata magonjwa mbali mbali kama vile;
• Ugonjwa wa Kipindupindu
• Shida ya kuharisha kila Mara
• Ugonjwa wa homa ya matumbo,typhoid
• Maambukizi ya Hepatitis A n.k
Watu kuumwa matumbo kila mara,kuharisha,kutapika, kupata UTI za Mara kwa mara,
Na wakati mwingine magonjwa kama Fangasi n.k, kutokana na uchafu.
Hivo moja ya Vitu vya Kuzingatia ili kujikinga na magonjwa mbali mbali kama nilivyoorodhesha hapo juu, ni Swala la Usafi wa Mazingira pamoja na kuhakikisha Unapata maji SAFI na SALAMA kila wakati.
Kwa Mujibu wa WHO; Inakadiriwa watu bilioni 2, robo moja ya watu duniani, hawana maji safi ya kunywa