Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mbali na uchafu kuganda kwenye Meno,Pia matumizi ya Pombe,marijuana n.k huweza kuharibu meno

Mbali na uchafu kuganda kwenye Meno,Pia matumizi ya Pombe,marijuana n.k huweza kuharibu meno

FAHAMU:Mbali na uchafu kuganda kwenye Meno kuwa chanzo kikubwa cha tatizo la Meno kwa watu wengi,

Pia wataalam wa afya ya kinywa na meno pamoja na tafiti mbali mbali za hivi karibuni zinaonyesha kwamba,

matumizi ya dawa mbali mbali za kulevyia, Marijuana,Unywaji wa Pombe hasa Pombe za Kienyeji kama vile GONGO huweza kuchangia kwa kiasi kikubwa tatizo hili la Meno,

Utafiti: Kutokana na tafiti hii ambayo imefanywa mwezi huu na jumuiya ya afya ya Meno ya Marekani yaani American Dental Association,inasema;

Nusu ya wataalam wa meno(dentists) wanasema wagonjwa ambao wameonekana kwenye Appoitnments zao,wengi wao wanatumia marijuana au dawa zingine,

Soma chapsho hili;

“Half of dentists say patients have shown up to appointments high on marijuana or another drug, according to survey results released this month by the American Dental Association”.

Pia Uvutaji wa Sigara huweza kuharibu Meno yako pamoja na Fizi zake.

USHAURI;

– Epuka matumizi ya Dawa za kulevyia

– Dhibiti matumizi ya Pombe kwa ajili ya afya yako, mbali na athari nyingi za Pombe kama vile kusababisha Ini kushindwa kufanya kazi,tatizo la Cirrhosis n.k,

Pombe pia huweza kuharibu meno yako

– epuka uvutaji wa Sigara,Tumbaku,matumizi ya UGORO,marijuana,coccaine au dawa zingine za Kulevyia

– Hakikisha unasafisha meno yako vizuri, fanya Usafi wa kinywa na meno kila mara,

Kumbuka; Uchafu kuganda kwenye meno,huweka meno yako kwenye hatari zaidi ya kushambuliwa na vimelea vya magonjwa mbali mbali.

#afyayameno #afyaclass

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.