Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MWANAMKE KUPATA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA( Tatizo kwa Wanawake wengi)

Maumivu wakati wa tendo kwa wanawake

• • • • • •

MWANAMKE KUPATA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA( Tatizo kwa Wanawake wengi)

Wanawake wengi wanalalamika juu ya tatizo hili pasipo kujua sababu hasa ya shida hii ni ipi.

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mwanamke kupata maumivu makali wakati wa tendo la Ndoa.

SABABU ZA MWANAMKE KUPATA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA NI PAMOJA NA;

– Hali ya ukavu ukeni ambayo huweza kusababisha hali ya  msuguano mkali,michubuko, na vidonda, mwisho wa siku mwanamke hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

– Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile UTI,FANGASI pamoja na maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke yaani PID

– Tatizo la mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani Hormone imbalance.

Fahamu kwamba katika sehemu za siri za Mwanamke kuna Tezi ambalo hufanya kazi ya kuzalisha maji maji,uteute na kuleta hali ya unyevu na ulaini ukeni,kwani sehemu za siri za mwanamke katika hali ya kawaida hazitakiwi kuwa kavu.

Hivo basi mabadiliko ya vichocheo mwilini huweza kuathiri utendaji kazi wa tezi hili,kwani linafanya kazi chini ya udhibiti wa vichocheo vya mwili au hormones.

– Matumizi ya baadhi ya kemikali wakati wa kuoga na wakati wa tendo la ndoa.

Baadhi ya kemikali ambapo zingine zipo kwenye sabuni za kuogea huweza kusababisha hali ya mabadiliko makubwa ya mazingira ya ukeni,

ikiwa ni pamoja na kuleta hali ya ukavu pamoja na maumivu makali wakati wa tendo la Ndoa.

Soma Zaidi hapa kuhusu chanzo cha maumivu wakati wa tendo kwa wanawake;

maumivu wakati wa tendo kwa wanawake

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo kwa wanawake, na sababu hizo ni pamoja na;

1. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya Zinaa,

Magonjwa ya Zinaa(sexually transmitted infection (STI)) huweza kuwa mojawapo ya chanzo cha maumivu wakati wa tendo kwa wanawake,

Yapo magonjwa mbali mbali ya Zinaa ambayo huweza kusababisha tatizo hili la maumivu wakati wa tendo kwa wanawake,magonjwa hayo ni pamoja na;

  • Ugonjwa wa Pangusa(chlamydia)
  • Ugonjwa wa Kisonono(gonorrhoea)
  • Maambukizi ya genital herpes n.k

2. Maambukizi ya Fangasi sehemu za Siri,

Fangasi pia huweza kuwa chanzo cha maumivu wakati wa tendo kwa wanawake

3. Maambukizi ya Bacteria kwenye via vya Uzazi vya Mwanamke,

Maambukizi haya kwa kitaalam hujulikana kama Pelvic inflammatory disease(PID).

PID ni mojawapo ya sababu kubwa ya maumivu wakati wa tendo kwa wanawake.

4. Mabadiliko ya vichocheo mwilini(hormonal changes)

Mfano kwa mwanamke akiwa kwenye kipindi cha Ukomo wa hedhi(menopause), mabadiliko makubwa ya vichocheo ambayo hufanyika kipindi hiki huweza kusababisha uke kuwa mkavu zaidi,

Hali hiii huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo kwa wanawake.

5. Mwanamke Kukosa hamu ya tendo,

Mwanamke kuwa na tatizo la kukosa kabsa hamu ya tendo ambapo huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo mabadiliko ya vichocheo mwilini,

Hali hii huweza kupelekea tatizo la Ukavu ukeni pamoja na maumivu wakati wa tendo kwa wanawake.

6. Kuwa na tatizo la kubana misuli ya Uke(vaginismus)

Vaginismus ni tatizo ambalo huhusisha kubana kwa misuli ya Ukeni, hali ambayo huweza kupelekea maumivu wakati wa tendo kwa Mwanamke au kushindwa kabsa kufanya tendo.

7. Kupata tatizo la Mzio(allergy),

genital irritation au allergy huweza kusababishwa na matumizi ya vitu mbali mbali ikiwemo dawa za kuua manii(spermicides), latex condoms au products mbali mbali kama vile baadhi ya Sabuni, shampoo n.k,

Shida hii ya Genital Irritation au allergy huweza kusababisha tatizo la maumivu wakati wa tendo kwa wanawake.

8. Sababu zingine za maumivu wakati wa tendo kwa wanawake;

  • Mwanamke kuwa na tatizo la Uvimbe kwenye kizazi,shida ya endometriosis n.k
  • Uvimbe kukua karibu na Uke au mlango wa kizazi(Cervix)
  • Kuwa na shida ya irritable bowel syndrome (IBS)
  • Shida ya kupata choo kigumu au constipation n.k

Hizo ndyo baadhi ya Sababu za maumivu wakati wa tendo kwa wanawake.

Matibabu ya Maumivu wakati wa tendo kwa Wanawake

Habari njema ni kwamba tatizo hili linatibika na kuisha kabsa. Ikiwa una tatizo hili la kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa, hakikisha unapata Msaada wa matibabu au;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Rejea Za Mada;

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.